📌SALMA HAROUN.
JESHI la Polisi limemtia mbaroni Nasra
Khalifa mwenye umri wa miaka 24 ambaye anatuhumiwa kwa kosa la kumuuwa na kumtupa
mtoto mchanga katika maeneo ya Uhindini Jijini Dodoma anaye kisiwa kuwa na
masaa machache duniani.
Akizungumza katika mahojiano maalumu
kamanda wa jeshi la polisi, Martini Otieno amesema mtuhumiwa huyo alifika
katika Hospitali ya Makole kwa kudai kusumbuliwa na matatizo ya tumbo na kuomba
kuelekea chooni ambapo alikaa kwa mda mrefu hali ambayo iIiuwatia hofu wauguzi.
Amesema wauguzi walifanikiwa
kumkuta mtuhumiwa huyo akiwa amejifungua mtoto wa kiume na kufanya jitihada za
kumtumbukiza katika tundu la choo.
Sababu iliYosababisha mtuhumiwa kufanya hivyo ni kutokuwa na maelewano mazuri kati yake na mwenzake hali ambayo imemsababisha kufanya tukio hilo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa
huo, Alnoor Kassam ameonesha kusikitishwa na tukio hilo na kukemea vikali watu
wanaotenda vitendo hivyo.
Hata kama umeachika kuna utaratibu wake wa kufanya lakini sio kutupa mtoto
Naye Mkazi katika mtaa huo, Muslim Mohammed
ameoneshwa kuumizwa huku akiomba serikali kuchukua hatua kali kwa baadhi
ya watu wenye kutenda vitendo hivyo
nchini.
Amesema sheria kali zichukuliwe kwa
baadhi ya watu wanaotenda vitendo hivyo ili viwe fundisho kwa watu wengine.
Tuendelee kukemea suala hili liishe hata kama mtu ana dhiki za maisha ajue kupambana nazo kuliko kufanya ukatili kama huu
0 Comments