WIZARA
ya Kilimo imeongeza bajeti ya utafiti na uzalishaji wa mbegu za awali kutoka
shilingi Bilioni 11.63 kwa mwaka 2021/2022 hadi shilingi Bilioni 40.73 kwa
mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 250.
Hayo
yamesemwa leo jiji Dodoma na Meneja wa mawasiliano na menejimenti ya maarifa wa
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Richard Kasuga wakati
akizungumza na waandishi wa habari amesema bajeti hiyo itaweza kutumika
kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora kwa kuongeza uzalishaji wa mbegu za awali
za mazao ya nafaka.
Mkurugenzi
huyo amesema TARI imepanga kuzalisha teknolojia mpya zikiwemo aina za mbegu
zenye sifa zaidi ya zile zinazotumiwa kwa sasa.
Aina hizo za mbegu zinasifa ya kutoa mavuno mengi, kustahimili ukame, ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu zenye viinilishe vingi pamoja na sifa zingine za soko kama vile sifa za mezani.
Teknolojia zingine zitakazogunduliwa ni za uongezaji thamani katika mnyororo wa thamani wa mazao, kuboresha afya ya udongo, kugundua mbinu bora za ukuzaji wa mazao, zana bora za Kilimo, na utunzaji wa mazao baada ya mavuno.
Aidha
Dkt. Richard Kasuga amesema Taasisi imepanga kuboresha maabara ya udongo katika
kituo cha TARI mlingano ili iweze kupata ithibati ya kimataifa.
Katika
mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya teknolojia 35 zitazaliswa, kati ya hizo 15 ni
mbegu bora, 5 agronomia, 5 afya ya udongo na 10 teknolojia baada ya mavuno.
0 Comments