📌AGNESS PETER
WANAWAKE wa mtaa wa Ilazo Jijini Dodoma wametakiwa kuunda vikundi vya watu watano na kujisajili katika ofisi ya serikali ya mtaa huo ili kupata mikopo iliyotolewa na Serikali kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa mtaa wa Ilazo Moses Mazengo,
leo Jijini Dodoma ambapo amewataka wanawake kujitokeza na kutumia fursa hiyo ya
kupata mikopo ili iwasaidie katika kukidhi mahitaji yao.
Moses amesema Serikali inatoa mikopo isoyokuwa na riba
lakini bado muitikio ni mdogo kutokana na masharti yaliyowekwa wakati wa
kuchukua fedha hizo.
Imekuwa changamoto kwa akina mama kutokana na masharti yaliyopo, wanashindwa kujisajili ili Serikali iwatambue maana hata fedha zinapotoka zinatakiwa kujulikana zinaenda kwa akina nani. Serikali inataka kutambua kama mtu anataka mkopo, ana malengo gani au vyanzo vya biashara yoyote? ndio sababu usajili unatakiwa.
Amesema serikali inashauri viundwe vikundi na vianze
kujiendesha kabla ya kuchukua mkopo ili kutengeneza vyanzo vya biashara na si
kusubiri fedha ya Serikali ndiyo ianzishe mtaji.
Kwa upande wake Lilie Samson ambaye ni mkazi wa eneo
hilo amesema kutokana na mikakati ya kupata mikopo hiyo ni mrefu hivyo
inapelekea wengi wao kushindwa kujisajili.
Amesema ni rahisi kujiunga na vikundi vya akinamama vya mtaani kutokana na taratibu zake hazihitaji mambo mengi kama ilivyo kwa Serikali
Inatakiwa kuunda kikundi cha watu watano baada ya hapo tunatakiwa kumfata bibi maendeleo wa mtaa atoe maelekezo ya namna ya kujisajili kisha kuandika barua ambazo zinatakiwa kwenda manispaa na kusubiri fedha kutoka kwa Mwenyekiti baada ya kujulikana Serikalini.
Aidha Christopher Peter mkazi wa eneo hilo, amesema
akinamama wanashindwa kujiunga na vikundi kupata mikopo ya serikali kutokana na
kushindwa kutengeneza malengo ya fedha hizo na kutokuwa na vyanzo vya biashara
ya kuzalisha fedha.
0 Comments