📌JOSEPHINE
MTWEVE
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa
mkoa wa Njombe kujitokeza kuhesabiwa Agosti 23 mwaka huu kwa lengo la kuisaidia
serikali kupanga majukumu yake kutokana na idadi ya watu.
Ameyasema
hayo wakati akikagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ambapo
amesema kuwa kutokana na takwimu ya watu na makazi itaisaidia serikali katika
usambazaji wa madawa.
Rais
Samia amesema kwa sasa serikali inasambaza madawa katika hospitali mbalimbali
nchini na bado hazitoshi kwasababu idadi ya watu imeongezeka kwa asilimia
kubwa.
Niwaombe mjitokeze kuhesabiwa kwasababu mambo yote tunayapanga kutokana na idadi ya watu mkijificha kuhesabiwa tutakuwa tunaleta kidogo ambacho hakitawatosha na wewe uliyejificha utakua unatumia cha mwenzio ambaye alihesabiwa.
Nawaomba wote tukahamasishane kwa hali yoyote mtu aliye mzee, mkongwe, mlemavu, mzima miaka yetu wote tukahesabiwe li mtupe fursa serikali yenu ya kujipanga vizuri
Aidha
Rais Samia ameongeza kuwa serikali ipo kwa lengo la kuwatumikia wananchi ambapo
amesema wanakwenda kujenga barabara kwa kiwango cha rami ama kwa kiwango cha
kupitika mwaka mzima.
Kwa
upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe
Dkt.Winifredi Kyambile amesema kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kulaza
wagonjwa mpaka 400 tofauti na awali.
Dkt.Kyambile
amesema kuna majengo mengine yatakayoongezeka kama vile Chuo kwaajili ya
kufundisha wataalamu watoa huduma ya afya pia kujenga nyumba kwaajili ya
watumishi.
Kukamilika kwa mradi huu kutaimarisha afya ya wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa ya jirani ambapo mwanzo tulikua tunawapeleka wangojwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya
Naye
Waziri wa Afya Ummi Mwalimu ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Njombe kujiunga
na Mfuko wa Bima ya Afya ili waweze kupata huduma za afya bila kikwazo.
0 Comments