WAMILIKI WA VIWANJA ILAZO WAMETAKIWA KUSAFISHA VIWANJA VYAO.

 

📌JOSEPHINE MTWEVE & SALMA HAROUN

WAMILIKI wa viwanja mtaa wa Ilazo Jijini Dodoma wametakiwa kusafisha viwanja vyao ili kuepukana na vitendo vya kiuharifu vinavyofanyika katika eneo hilo.

Hayo yameyasemwa leo na Mwenyekiti wa mtaa huo Moses Mazengo ofisini kwakwe ambapo amesema viwanja hivyo vimekua na vichaka vingi hali yakuwa wamiliki wanaviona na hawachukui hatua ya kuvisafisha.

Amesema vichaka hivyo vimekua chachu ya kuficha wahalifu katika eneo hilo huku hatari kubwa ikiwa ni kwa watoto wa kike ambao wamekua wakitembea majira ya usiku.

Vichaka ambavyo viko katika maeneo mbalimbali hapa Ilazo ni tishio kubwa sana kwasababu wahalifu wengi hujificha humo hasa majira ya usiku na kupelekea watu kutoishi kwa amani katika maeneo yao

Kwa upande wake Mariam Peter ambaye ni mkazi wa Ilazo amesema vichaka hivyo vimekua tishio kwa wakazi wa eneo hilo ambapo matukio mengi ya kiuhalifu yamekua yakitokea.

Mariam amewaomba wamiliki wa viwanja hivyo waweze kuvisafisha kwani ni hatari kwa maisha hasa kwa watoto wakike.

Kwa kweli vichaka hivi vimekua kero sana kwetu unakuta mtu umetoka kazini usiku unarudi nyumbani ukapumzike lakini njiani unakutana na vibaka wanakupora kila kitu

Ramadhani Ally ni miongoni mwa wamiliki wa viwanja hivyo amesema moja ya sababu zinazowafanya wamiliki wengi washindwe kusafisha viwanja vyao ni kutokaa katika maeneo hayo.

Ally amesema wamiliki wengi wamekua wakitoka sehemu tofautitofauti na si wakazi wa eneo hilo hivyo maeneo mengi yamekua na vichaka kutokana na wahusika kutotembelea viwanja vyao mara kwa mara.

Naomba sheria kali iwekwe kwa wamiliki ili kupunguza hii tabia ya watu kuvitelekeza viwanja vyao ukizingatia Ilazo iko Dodoma mjini kabisa lakini kumekua na vichaka vingi na watu hawasafishi maeneo yao


Post a Comment

0 Comments