WAKAZI WA JIJI LA DODOMA WATOA MAWAZO YAO JUU YA ZOEZI LA SENSA

 

📌JOSEPHINE MTWEVE & SALMA HAROUN

AGOSTI 23 mwaka huu ni siku iliyoridhiwa kuwa ya mapumziko na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambapo wananchi wote walitakiwa kubaki nyumbani kwaajili ya mapumziko ili kuhesabiwa. Lakini baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wametoa malalamiko yao juu ya makarani kutojitokeza kwa wakati katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa leo na Mwanahamisi Juma wakati wa mahojiano maalumu, amesema wameweza kuathirika na mapumziko hayo kutokana na kutofanya shughuli zao za kila siku.

Mwanahamisi amesema kuwa hawajaona umuhimu wa kutenga siku hiyo kwaajili ya mapumziko kutokana na makarani kutofika maeneo husika kwa wakati.

Naiomba serikali kuwahamasisha makarani kufanya kazi kwa bidii kwasababu baadhi yao tunapishana nao mitaani na inapelekea sisi wananchi kudhani kuwa hakuna umuhimu wa zoezi hilo

Kwa upande wake Kelvin Mosha amesema wameweza kutii agizo hilo kwa kukaa nyumani kusubiri uhesabuji huo huku wakipoteza muda wao ambao wangeutumia kwaajili ya kujipatia kipato.

Amesema serikali iweke makarani wengi zaidi ili kuweza kufanikisha zoezi hilo kwa urahisi zaidi.

Mimi nimeweza kuwasubiri makarani tangu asubuhi lakini mpaka jioni hawakutokea wakati huo ningekua kwenye shughuli zangu ningeweza kujiingizia kipato lakini sio kukaa tu nyumbani bila kufanya chochote

Kwa kuwa si rahisi kumaliza zoezi hili kwa siku moja, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulu Hassani amewataka wananchi kutunza kumbukumbu za watu wote waliolala katika kaya zao usiku wa tare 23 Agosti mwaka huu ili karani atakapopita azikute ili aziingize katika mfumo wa kukusanyia taarifa kwani zoezi hili ni endelevu.

 

Post a Comment

0 Comments