WAFANYABIASHARA WAASWA KUTENGENEZA VIKUNDI VYA KUWEZESHANA KIFEDHA.

 

📌AGNESS PETER

WAFANYABIASHARA wa Soko la sabasaba jijini Dodoma wameshauriwa kutumia fursa za kuunda vikundi vya kuchangiana na kukopeshana fedha kwa lengo la kujinufaisha na kukuza biashara zao ili kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa leo na Katibu mkuu wa eneo hilo Nyamsuka Wisaka ambapo amewataka kuwa huru kujiunga na vikundi hivyo ili kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali za kibiashara.

Nyamsuka amesema hamasa inayotolewa kwa wafanyabiashara ni kubwa kulingana na soko hilo kuwa na watu zaidi ya elfu saba.

Kuna vikundi zaidi ya ishirini hadi thelathini ambavyo vimesajiliwa kisheria mfano kuna kikundi kinaitwa TWIGA kilichozinduliwa na Mkuu wa Wilaya na Mbunge chenye watu zaidi ya 30 ambacho kinachangiana fedha kwaajili ya mambo mengi hata ya kijamii kama ugonjwa vifo na majanga mengine

Nyamsuka.

Kwa upande wake Ismail Saidy ambae ni mfanyabiashara wa nguo katika Soko la Sabasaba amewataka wafanyabiashara wengine kutumia njia za kujiunga na vikundi vilivyoanzishwa katika kukuza biashara zao na kujikwamua kiuchumi.

Amesema biashara nyingi zinahitaji mikopo ili kukua hivyo vikundi vinahitajika kwa lengo la kusaidiana kiuchumi na kijamii kwa ujumla.

Katika soko hilo vikundi vipo vingi lakini pia kuna benki ndogondogo ambazo huwa zinakuja kutoa elimu juu ya mikopo na kutoa mikopo kwa wafanyabiashara ambayo huwa inatusaidia

Aidha mfanyabiashara wa mbogamboga Selina Andason amesema baadhi yao hawapendi kujiunga na vikundi na kukopa mikopo kutokana na kuogopa kutengeneza madeni yatakayosababisha kuanguka kwa biashara zao.

Post a Comment

0 Comments