VIPAUMBELE WIZARA YA MAJI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023

SAIDA ISSA

WIZARA ya Maji  imetaja vipaumbele vyake katika  mwaka wa fedha 2022/2023 kuwa ni  usimamizi wa rasilimali  za maji, usimamizi wa ubora wa maji, ujenzi wa miundombinu ya  utoaji wa huduma ya maji vijijini, uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira mijini pamoja na uimarishaji wa taasisi za sekta ya maji.

Hayo yamesemwa leo Agosti 12 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati akitoa taarifa ya Wizara kuhusu vipaumbele katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.

Amesema Wizara ya maji  imeidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 709,361,607,000 kwaajili ya matumizi, na kati ya fedha hizo matumizi ya kawaida ni shilingi bilioni 51,462,269,000 ambapo shilingi  16,700,534,000 ni kwaajili ya kugharamia matumizi mengineyo na shilingi 34,761735,000 ni kwaajili ya  kulipa mishahara ya watumishi wa Wizara.

RUWASA na  Chuo cha Maji kwa upande  wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo fedha zilizotengwa ni shilingi ni Bilioni 657,899,338,000 zikihusisha shilingi Bilioni 407,064,860,000 fedha za ndani  na shilingi  billion 250,834,478,000 ni za nje

Mahundi

 Akizungumzia kuhusu usimamizi wa rasilimali za maji zilizopo nchini amesema zinakadiriwa kuwa na mita za ujazo billion 126 kwa mwaka zikiwemo bilioni 105 juu ya ardhi na billion 21 chini ya ardhi.

Serikali katika mwaka 2022/23 itaendelea kuwekeza katika  utunzaji wa vyanzo vya maji, ujenzi wa miundombinu ya kuongeza upatikanaji wa maji kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Mahundi

Amesema kuhusu usimamizi wa ubora wa maji  safi na salama kwa wananchi waishio vijijini inafika zaidi ya asilimia 85 ifikapo mwaka 2025 Wizara imepanga kutekeleza  jumla ya  miradi  1029 ya maji ambapo miradi 648 ni miradi inayoendelea kutekelezwa na miradi 381 ni mipya.

Aidha katika uboreshaji  wa upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira  mijini amesema imepanga kutekeleza jumla ya miradi yenye kulenga kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waishio mijini.

Mhandisi Mahundi amesema  katika uimarishaji wa Taasisi za sekta ya Maji  Wizara imejipanga  kuwa na wataaalamu wa kutosha  na wenye weledi wa hali ya juu, Serikali itaendelea kukiimarisha na kukitumia chuo cha maji ili kutoa wataalam wa maji watakaotumika katika usimamizi wa uendeshaji wa miradi ya maji hususani ya vijijini pamoja na kufanya tafiti za kutatua changamoto mbalimbali za sekta ya maji.

Mamlaka  za maji na usafi wa Mazingira vijijini RUWASA bodi ya Taifa ya Maji na Bodi za Mabonde  za maji zitaimarishwa ili kuhakikisha mipango iliyopo inafikiwa

Mahundi

  

Post a Comment

0 Comments