UWANJA WA NDEGE IRINGA KULETA WATALII WA KUTOSHA.

📌JOSEPHINE MTWEVE

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kutumia ipasavyo miundombinu ambayo inatekelezwa katika Mkoa kwaajili ya kukuza uchumi.

Ni katika uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi uwanja wa ndege leo mkoani Iringa ambapo amesema miradi yote inayotekelezwa hususani uwanja huo ni kwaajili ya kukuza biashara ndani na nje ya nchi.

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa uwanja huo utaweza kuleta utalii wa kutosha katika mkoa huo kutokana na kuwepo kwa vivutio vingi vya utalii.

Iringa tuna vivutio vingi vya utalii ambavyo bado havijafunguliwa kwa utalii lakini Iringa kuna kituo cha utalii hatujakiendeleza lakini mnajua tuna mradi mwingine wa rigro.

Kuwepo kwa mradi wa rigro unakwenda kujenga kituo cha utalii ambacho kwa mda mrefu kimeachwa sasa miradi hii kituo cha utalii, uwanja wa ndege na kuna miradi ya barabara ambayo tunakuja kujenga Iringa wakandarasi wako mbioni kutafutwa ili waje kujenga barabara ikiwemo barabara inayokwenda mbuga ya Ruaha

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara TANROADS Injinia Rogatus Mativila amesema kuwa kiwanja cha Iringa ni moja ya viwanja vinavyomilikiwa na kuendeshwa na serikali ambapo kilianza kutumika mwaka 1950.

Amesema kiwanja hicho kimekua kikihudumia abiria wa ndani na wageni wanaotembelea hifadhi ya taifa ya Ruaha na serikali imekua ikikifanyia marekebisho mara kwà mara kwaajili ya usalama wa abiria.

Ujenzi wa uwanja huo unapata fedha kutoka maeneo mawili ambapo serikali inakwenda kujenga uwanja kwa maana barabara za kutua na kurusha ndege kwa asilimia 100% na ujenzi wa jengo la abiria la kupokea na kusafirisha litajengwa kwa mkopo wa benki ya dunia 

Post a Comment

0 Comments