KITUO cha Uwekezaji
Tanzania (TIC) Kanda ya kati Dodoma kinatoa wito kwa vijana kufanya uwekezaji
kupitia fursa mbalimbali pamoja na kutoa elimu kupitia warsha na semina kwa
wajasiliamali wadogo, wakati na wakubwa kwa lengo la kuwajenga kitaalamu.
Hayo yamesemwa leo jijini
Dodoma na Kaimu Meneja wa Kituo cha uwekezaji Kanda ya kati Juma Ally Nzima
ambapo amesema kupitia kituo hicho vijana wamenufaika kwa kuwezeshwa kutazitambua
fursa mbalimbali zilizopo ambazo zina manufaa ikiwa ni pamoja na sekta ya
kilimo.
Nzima amesema kupitia
taasisi mbalimbali wanatoa elimu kwa umma hasa vijana ili kuwapa uwezo wa
kupata taarifa tofauti na kufanya zana nzima za uwekezaji.
Kwa muktadha wa TIC uwekezaji ni shughuli ya kiuchumi ambayo lengo lake ni kuwekeza fedha kwaajili ya kupata faida na kutengeneza ajira na kuinua uchumi wa nchi kwa mawanda mapana
Aidha amesema moja ya
jukumu la kituo hicho ni kuishauri serikali kuhusu Sera rafiki za uwekezaji
nchini kwa lengo la kukuza uwekezaji nchini.
Kwa upande wake Emmanuel
Paulo ambae ni mkazi wa Jiji la Dodoma ameomba serikali kuangalia namna ya
kuwawezesha vijana kupata kipato cha uwekezaji kutokana na changamoto za vipato
hasa kwa wale wanaotoka vyuoni.
Amesema muitikio kwa
vijana katika uwekezaji ni mdogo kutokana na uhaba wa elimu ya kutosha juu ya
suala hilo hivyo taasisi husika ziongeze nguvu ya kutosha katika utoaji
mafunzo.
Jenipha Antony mkazi wa Jiji
la Dodoma ameiomba serikali kutoa ajira kwa wingi ili kupunguza ongezeko la
vijana wasio na ajira mtaani kwa lengo la kuwapa uwezo wa kujiwekeza katika
sekta mbalimbali pamoja na kupata mikopo ya kuanzisha biashara.
Nipende kuishauri taasisi ya TIC waweze kufanya jitihada za kuwafikia vijana popote pale wanapokuwa wanapatikana iwe mjini au ndani vijijini watu wanashindwa kufikiwa na kupewa elimu kwahiyo kama wataweza kuwafikia hawa vijana itakuwa fursa kubwa kwao
TIC ni taasisi ya Umma
yenye jukumu la kuhamasisha, kuhimiza, kufanikisha, kuratibu masuala ya
uwekezaji pamoja na kufanya shughuli mbalimbali za kutangaza fursa ndani na nje
ya nchi kwa lengo la kukuza uwekezaji Tanzania.
0 Comments