📌SALMA HAROUN & AGNESS
PETER
MKURUGENZI Mkuu wa Tume
ya TEHAMA Dkt.Nkundwe Mwasaga amesema kazi kubwa ya TEHAMA ni kuratibu
utekelazaji wa sera ya taifa pamoja na kukuza huduma za TEHAMA kwa lengo la kuwafikia
wananchi.
Ameyasema hayo leo wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema sehemu ya
kukuza huduma hizo inahusisha sekta binafsi zinazofanya shughuli zake kwa
kutumia TEHAMA ambazo zinaweza fanywa ndani na nje ya Tanzania.
Dkt.Mwasaga amesema wanaangalia Mikoa imejiandaa vipi katika mabadiliko ya kidigiti ili kuhakikisha shughuli zote za kibiashara na za kijamii zinafanyika katika mitandao ili kukuza mapato ya mikoa na wengine kutengeneza ajira.
Tunahakikisha Tanzania inapambana na nchi zingine kwenye uchumi wa dunia kuhakikisha kwamba uchumi wetu unakua uchumi wa ushindani
Aidha Dkt. Mwasanga
ameongeza kuwa lengo kubwa ni kukuza wanataalamu, kampuni ndogondogo, mikoa ili
kuhakikisha mikoa inashindana na kuifanya Tanzania iweze kushindana na nchi
nyingine kwenye uchumi mkubwa wa kidigiti wa dunia.
Naye Msemaji Mkuu wa
Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amewataka
vijana kujitokeza katika kuchangamkia fursa za TEHAMA
Amesema tume ya taifa ya
TEHAMA imejiandaa vyema katika kuhakikisha Tanzania inakua katika mfumo wa
kidigiti ambapo itaweza kurahisisha shughuli za kiuchumi.
0 Comments