📌JOSEPHINE MTWEVE
SERIKALI imeombwa kupitia upya muundo mpya wa
utawala wa Mamlaka za Serikali za mitaa Tanzania wa mwaka 2022 ambao umetajwa
kutotendea haki upande wa uuguzi na ukunga kwa lengo la kuboresha na kutoa
huduma zilizobora kwa uangalizi stahiki.
Hayo yamesemwa na Alexander
Mauliya ambae ni Raisi wa Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA) ambacho ni Cha
kitaaluma kinachotetea na kushirikiana na Serikali kushawishi kutengeneza
mazingira rafiki kwa wanataaluma amesema baada ya kupitia muongozo huo na
kushauriana na wadau mbalimbali waliona haujatendea haki taaluma ya uuguzi na
ukunga.
Amesema
changamoto za afya zipo nyingi lakini huenda zinaweza kuongezeka endapo muundo
huo utaendelea kutekelezwa na utatoa fursa ya kukosa usimamizi bora wa kazi kwa
ukaribu kutokana na kutotambulika katika ngazi za halmashauri.
Mfano unaposhindwa kutambua muongozo wa Wauguzi katika halmashauri za mikoa nani atakayesimamia ambae atakuwa anajua changamoto iliyotokea ya kitaaluma? sasa leo unapoondoa Mamlaka za kiutawala kwenye halmashauri zetu za uuguzi na ukunga tafsiri yake unaenda kudhoofisha huduma ambazo sisi tumeziona za muhimu sana
Amesema
idara iliyokuwepo mwanzoni ilikuwa ikisimamiwa na mganga mkuu wa Wilaya ambae
alikuwa akisimamia kada zote zilizo chini yake zinazohusika na masuala ya afya
lakini kutokana na maboresho ya muundo huo mpya huduma ya uuguzi na ukunga
haijatambulika.
Aidha
ameiomba Serikali kusitisha muundo huo na kufanyia kazi mapendekezo yao ambayo
yaliwasilishwa mwezi Mei 31 mwaka huu baada ya kilele cha maadhimisho ya uuguzi
na ukunga duniani ambapo waliahidiwa kufanyia kazi.
Hatukuishia hapo tuliwaandikia Wizara husika mapendekezo yetu lakini mpaka muda huu hatujapata mrejesho na tulifanya jitihada za kuuona uongozi wa Wizara hatujafanikiwa
Hata
hivyo amesema chama kiko tayari kuitwa kukaa pamoja na Wizara husika kujadili
na kushauriana ili maboresho yawe shirikishi, Ili wanapoenda kujipanga
kuhudumia jamii kila mtu awe anajua wajibu wake na stahiki zake na nini
kifanyike hatimaye waweze kutoa huduma zilizo bora.
0 Comments