SHIRIKA
la huduma ya viwanda vidogo (SIDO) imetoa msukumo kwa wajasiriamali
wanaojiwekeza katika maeneo ya kuzalisha mitambo na vitendea kazi mbalimbali kutumia
fursa ya kupata elimu kupitia taasisi hiyo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi
Taasisi
ya SIDO imejiratibu katika kutimiza wajibu wa kuanzisha na kuendeleza viwanda
katika sekta ya teknolojia kwaajili ya kuhakikisha wajasiriamali wanapata
mahitaji stahiki yanayohitajika
Hayo
yamesemwa leo jijini Dodoma na Mratibu wa miradi (SIDO), Stephano Martini Ndunguru
ambapo amewataka vijana kuambatana na taasisi hiyo katika kupata mafunzo ya
ujasiriamali kwa lengo la kuwafungua kimtazamo katika kuhakikisha wanaweza
kujihimili.
Aidha
amesema baada ya kumaliza mafunzo kwa wanaoshughulika na mazao au bidhaa
zinazohitaji kuthibitishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) watawaunganisha
nao ili kujiridhisha kuwa bidhaa zao zimekidhi viwango vya ubora kwa matumizi
sahihi.
Tunakuwa na eneo la mafunzo ya ujasiriamali na huduma za ugani na ni kwa nadharia na vitendo ambayo inalenga moja kwa moja kumfungua mjasiriamali au mtanzania yoyote katika mtazamo ili aweze kuhimili katika kuhakikisha mazingira yake yanamungiza kipato
Kwa upande wake Halphan Amini ambae ni fundi wa kuchomelea katika taasisi ya SIDO amewashauri vijana kutumia fursa za taasisi hiyo katika kupambana kufanya kazi ili kujikimu kiuchumi
Naye
Majaliwa Samweli aliyejiajiri mwenyewe amewataka vijana kusimama na kujitambua
kwa kujiajiri wenyewe kwa kutokutegemea serikali iwaajiri.
Ukionyesha kitu hata serikali inaweza kukutazama na kuweza kukusaidia lakini ukibaki mtaani na kubweteka hata watu watakutelekeza
0 Comments