KUFUATIA
Jiji la Dodoma kuendelea kukua baadhi ya wananchi wa jiji hilo wameiomba
Serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za maisha na kutoa elimu juu ya
kutumia fursa zilizopo kutokana na wengi wao kushindwa kunufaika nazo.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dodoma na baadhi ya wananchi ambapo Willson Masinga ambaye
anajishughulisha na shughuli za ujenzi amewataka vijana kuwa na fikra za haraka
katika kutambua nini kifanyike ili kuepukana na hali ngumu ya maisha.
Masinga
amesema kutokana na maisha kuwa magumu imepelekea watu wengi kushindwa kuweka
akiba kwasababu fedha nyingi zinatumika kupata mahitaji ya siku bila kubaki na
akiba
Kwasasa vitu vimepanda bei sana kiasi cha pesa tunazopata zinatosha tu kununua mahitaji ya nyumbani hasa kwa sisi tunaofanya kazi za kujenga tunashindwa hata kuweka akiba ya pesa angalau tatizo likitokea zitusaidie au tu akiba ya kuanzisha biashara
Aidha
Queen Samson ambae ni mfanyabiashara wa vifaa vya urembo ameiomba Serikali
kupitia ngazi za mitaa kutoa elimu ya namna ya kujiajiri kupitia fursa ya
muingiliano wa watu katika jiji hilo.
Amesema
wingi wa watu ni fursa mojawapo ya kujiajiri kwa kufanya biashara ambazo si
lazima Serikali itoe au iseme.
Hata
hivyo amesema wapo baadhi ambao ni ngumu kupata mawazo ya haraka kuhusu nini
kifanyike ili kutengeneza biashara kulingana na watu wa eneo husika hivyo
Serikali ina wajibu wa kusaidia kutoa elimu.
Watu wengi huwa wanasubiri Serikali iseme au itoe fursa fulani ndio watu wachangamkie lakini sisi wenyewe tunawajibu wa kufikiria kujiajiri wenyewe na kuwa wabunifu kwasababu fursa zinapatikana kwenye wingi wa watu japo hata Serikali inawajibu pia wakutoa elimu
Kwa
upande wake Hawa Sadock ameiomba Serikali kupunguza gharama za maisha ili
kupata urahisi wa kujiajiri na kuweka akiba pamoja na kukuza jiji hilo kupitia
shughuli za kiuchumi endapo bidhaa zitashuka bei.
0 Comments