SERIKALI YAAHIDI KUIMARISHA NA KUENDELEZA SANAA NA MICHEZO NCHINI

 

📌AGNESS PETER

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Zanzibar imeahidi kuimarisha na kuendeleza michezo nchini kwa  kujenga miundombinu bora ya michezo kwa shule za msingi na sekondari na kuendeleza katika vyuo vya elimu ya kati na elimu ya juu kwa lengo la kukuza vipaji vya michezo na taaluma za wanafunzi.

Ni katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora ambapo umefanyika ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingi UMITASHUMTA na umoja wa michezo kwa shule za sekondari UMISSETA ambapo Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuajiri walimu wa michezo ambapo kwa mwaka wa fedha 2022 2023 imeajiri walimu 83 na kuwapanga kufundisha katika shule teule zinazofundisha somo la elimu ya michezo.  


Amesema serikali inatambua umuhimu wa sanaa na michezo katika ukuaji wa maendeleo ya wanafunzi kiakili na kijamii kutokana na kuwa miongoni mwa stadi muhimu zinazochangia ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ikiwemo kutengeneza fursa za ajira .

Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu katika shule teule 56 nchini ikiwa ni wastani wa shule mbili kila mkoa ivyo nikiwa hapa nimefurahishwa na utekelezaji bora wa vituo vya michezo ikiwa ni viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana na shule ya sekondari ya wavulana Tabora

Amesema ujenzi wa miundombinu ya michezo utafanyika kwa awamu katika shule nyingine kikanda ikiwa na lengo la kuhakikisha kunakuwa na shule zenye miundombinu bora ya kuwezesha wanafunzi kusoma somo la elimu kwa michezo kikamilifu kwa nadharia na vitendo ili kuzalisha wataalam watakaobobea katika michezo.

 Leo tunafanya mashindano haya ikiwa ni miaka 22 imepita tangu kufanyika kwake ambapo mara ya mwisho kufanyika ilikuwa ni mwaka 1999 na tunatarajia kupokea wanamichezo kutoka UMISSETA 3497 na viongozi 703 kutoka pande zote mbili za muungano yaani Bara na Visiwani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora ameishukuru serikali kwa uteuzi wa mkoa huo kuwa mwenyeji wa mashindano ya michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA kitaifa kutokana na faida walizozipata kwa kuleta fursa za huduma kwa jamii na kwa wanamichezo.

Amesema mkoa huo umefanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuelimisha juu ya watoa huduma kutumia vizuri fursa za michezo katika kujipatia kipato na kuwahudumia wageni katika mazingira rafiki na ya upendo.

Naishukuru serikali kwa kutoa Billioni 767 Millioni 888 na 776 kwaajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya michezo katika shule yetu ya Tabora ya wavulana ambapo walipata Millioni 543,568,234 na kwa shule ya wasichana Tabora walipata Million 224,320,532 na ujenzi na ukarabati wa miundombinu inaendelea katika hali nzuri.

Aidha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Rizick Shemdoe amesema vitabu viwili vimeundwa ambavyo vimebainisha changamoto zilizopo katika shule za msingi na sekondari na kuweka mikakati ya namna maamlaka ya serikali za mitaa kuondoa changamoto hizo.

Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi UMITASHUMTA ulianzishwa mwaka 1970 na Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari UMISSETA ilianzishwa mwaka 1974 kwa lengo la kukuza vipaji vya michezo na taaluma za wanafunzi nchini.



 

 

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments