SEKTA YA UTALII TANZANIA KUONGEZA PATO LA TAIFA.

 ðŸ“ŒJOSEPHINE MTWEVE & SALMA HAROUN

NCHI ya Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya kitalii ambavyo vinasaidia kuongeza pato la taifa na kuendeleza ustawi wa maisha kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo katika hafla ya kukabidhi magari yanayotolewa na mradi wa REGROW Mikumi Mkoani Morogoro na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema sekta hii inachangia kwa robo ya fedha zote za kigeni zinazotokana na mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi. Hivyo sekta hiyo ikisimamiwa ipasavyo inaweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi na kuleta maendeleo.

Na ndio maana kipekee kabisa Mh. Samia ameweka kipaumbele cha juu sana kwenye sekta hii na hata kufanya jambo la kijasiri ambalo wengi hawakulifikiria, Mkuu wa nchi, Amirijeshi Mkuu yeye mwenyewe kuwa mmoja ya waigizaji wakuu wa ile sinema ambayo imetutoa kimasomaso kutangaza fursa za taifa letu

Aidha Dkt.Mpango ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita imeweza kuelekeza jicho lake katika sekta ya utalii.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana amesema Wizara itaendelea kusimamia utekelezaji wa mradi wa REGROW ili ufikie malengo yake kama ilivyopangwa.

Post a Comment

0 Comments