OFISI
ya Taifa ya Takwimu imetoa rai kwa taasisi zinazotoa huduma kwa watalii
kuendelea kuboresha zaidi huduma zao kutokana na umuhimu wa sekta ya utalii
katika kuingiza fedha za kigeni kwa lengo la kuwavutia watalii ambao
walishawahi kufika nchini.
Hayo
yamesemwa Leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Daniel Masolwa
wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema sekta ya utalii
inachangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 17 na kuchangia mapato katika
fedha za kigeni kwa takribani asilimia 25.
Amesema
idadi ya watalii kutoka nje ya nchi waliotembelea vivutio mbalimbali vya utalii
katika kipindi cha Januari hadi Julai mwaka huu waliendelea kuongezeka hadi kufikia
742,133 ikilinganishwa na watalii 456,266 walioingia nchini mwaka 2021 ikiwa ni
sawa na asilimia 62.7.
Watalii walioingia nchini mwezi Julai 2022 pekee waliongezeka hadi 166,736 ikilinganishwa na watalii 81,307 walioingia nchini mwezi Julai 2021 sawa na ongezeko la asilimia 105.1 na idadi ya watalii walioongezeka mwezi Julai 2022 ilikuwa zaidi ya mara mbili ya watalii walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2021
Aidha
amesema idadi kubwa ya watalii walioingia nchini kutoka nchi zilizo nje ya bara
la Africa kwa mchanganuo wa utaifa kwa kipindi cha Januari hadi Julai 2022
walitoka Marekani ikiwa na watalii 51,301.
Amesema
nchini watalii kutoka bara la Africa ambapo katika kipindi Cha Januari hadi
Julai walipokelewa kutoka Kenya kwa idadi ya watu 86,220, Burundi 54,877,
Malawi 27,079, Uganda 21,080 na Afrika kusini 20,868.
Katika kipindi cha mwezi Julai pekee mwaka huu idadi kubwa ya watalii walioingia nchini walitoka Kenya 16,654, Burundi 7,966, Malawi 5,113, Afrika kusini 4,335 na Rwanda 4,035
Kwa
mujibu wa Sera ya Mapitio ya Ofisi ya Takwimu, idadi ya watalii wanaoingia
nchini zinaweza kufanyiwa mapitio endapo Takwimu mpya na zilizohusishwa kutoka
kwenye chanzo zinapatikana.
0 Comments