KATIKA
jamii kumekuwa na asilimia kubwa ya watu wanaopitia ugumu wa maisha na kuishi
katika mazingira hatarishi kutokana na sababu tofauti za kimaisha na kupelekea
kupotea kwa malengo na ndoto walizozitarajia katika kufanikisha hilo.
Magreth
Magabila ni mwanamke aliyekuwa na ndoto za kuwa mama bora lakini mwenye
kujishughulisha kama watu wengine lakini ndoto hizo zilipotea mara baada ya
kupata ajali ya gari mwaka 2002 akitokea chuoni katika kijiji cha Homboro
Jijini Dodoma.
Akizungumza
wakati wa mahojiano amesema ajali ilisababisha kuumia kwa kiasi kikubwa upande
wa kichwani jambo lililomlazimu kufanyiwa upasuaji ili kunusuru maisha yake.
Sikuweza kupata malezi mazuri kutokana na kwamba nina mzazi mmoja ambae ni baba na mama ambae ni mama mdogo kwa hiyo hakulichukulia jambo la kidonda changu kichwani kwà uzito nikaanza kupata manyanyaso na kuambiwa nifanye kazi kama mtu ambae sijawahi kupata tatizo la aina yoyote
Licha
ya Magreth kuwa na tatizo la kichwa, aliporuhusiwa kurudi nyumbani na kupewa masharti
ya kulelewa kama mtoto mchanga lakini amesema alipata mateso makali alipokuwa
akiishi na wazazi wake jambo lililopolekea kutohimili hilo na kutoroka nyumbani
kwao.
Amesema
baada ya kutoroka alikutana na msamalia aliyetaka kumsaidia kumsomesha lakini
alipogundua ametoroka nyumbani alimshauri kurudi nyumbani kuomba msamaha kwÃ
wazazi wake kisha akampa nauli ya kumsafirisha.
Magreth
amesema kutokana na mama yake mdogo kuonekana kutopendezwa naye aliamua
kuondoka na kuolewa ambapo mwaka 2010 mwezi wa 9 mumewe alivamiwa na kujeruhiwa
vibaya katika biashara yake.
Mume wangu hakuugua sana alifariki mwezi huo huo na mateso yakaendelea kutokana na ndugu wa mume wangu kuninyang'anya hata vidogo nilivyokuwa navyo sikupata msaada wowote nikaanza kuhangaika
Kuanzia
mwaka 2014 Magreth amesema alipata tatizo jingine la uti wa mgongo ambapo mwaka
2018 alishindwa kabisa kutembea na mnamo tarehe 23 mwezi wa Februari mwaka huu
alipata msaada wa fedha za hospitali ambapo aligundulika kuwa pingili za uti wa
mgongo zimepinda.
Mpaka
sasa Magreth anaishi Dodoma kwa kutegemea msaada wa wasamaria wema pamoja na
watoto wake wawili wa kiume ambao ni wadogo kiumri na bado anahitaji msaada wa
fedha za matibabu ili aweze kujishughulisha na kuwajibika kama watu wengine.
0 Comments