📌JOSEPHINE MTWEVE &
SALMA HAROUN
MKUU wa Mkoa wa Dodoma
Mh. Rosemary Senyamule ameahidi kuendeleza jitihada zilizofanywa na aliyekua
mkuu wa mkoa huo Mh.Antony Mtaka mara baada ya kukabidhiwa ofisi katika
kutekeleza majukumu ya kiserikali.
Hayo ameyasema leo Jijini
Dodoma ambapo ameahidi kuendeleza ujenzi wa soko la machinga ambalo
litajumuisha wajasiriamali wa mkoa huo kwa lengo la kufanya biashara na kukuza
uchumi wa nchi.
Aidha amewaomba viongozi
wote wa Mkoa wa Dodoma kuyajua majukumu yao na kuyatekeleza ili kuweza
kukamilisha yale yote yaliyoanzishwa na aliyekua Mkuu wa Mkoa huo Mh. Mtaka ili
kuleta taswira nzuri katika Jiji la Dodoma.
Niombe ushirikiano wenu sana ili Dodoma hii inayotegemewa na watanzania iweze kuwa na sura inayotarajiwa
Kwa upande wake aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Antony Mtaka amemwomba aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa huo kuwapa vipaumbele vijana katika suala zima la fursa mbalimbali za kiofisi.
Amesema vijana wengi
waliokua wamekosa ajira baada ya kumaliza masomo yao walijitolee kufanya kazi
bila malipo ili kuweza kupata uzoefu kwa lengo la kutengeneza mazingira ya
kupata kazi kwa urahisi.
Pia Mh. Mtaka
amewashukuru wale wote ambao ameshirikiana nao katika kipindi chote cha
majukumu yake mkoani Dodoma hususani waandishi wa habari kwa kufanya kazi
pamoja kwa lengo la kuhabarisha jamii.
0 Comments