KUFUATIA
kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuridhia
siku ya sensa kuwa ya mapumziko baadhi ya wafanyabiashara wa Jiji la Dodoma
wametoa maoni yao ni kwa kiasi gani wataweza kuathirika na mapumziko hayo.
Akizungumza
leo Shabani Ally ambaye ni mfanyabiashara wa nyama katika Soko kuu Majengo
amesema kuwa utaratibu huo umekua wa tofauti ukilinganisha na sensa zilizopita
ambazo zilikua zikiruhusu watu kwenda kufanya biashara zao.
Ally
amesema kutokana na biashara anayoifanya kuna changamoto ambayo ataweza kuipata
kutokana na kutofanya kazi siku hiyo hususani kwa wafanyabiashara wanaofanya
biashara za mali kuoza.
Kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza wateja kwasababu tuna wateja wanaokuja siku kadhaa katika wiki hivyo kwa wateja waliozoea kuja katika siku ya jumanne ambayo imegongana na siku ya sensa tutawapoteza
Kwa
upande wake Willison Mazinga ambaye anajishughulisha na shughuli za ujenzi
amesema kuwa itaweza kumwathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi yake
anayoifanya ni ya kulipwa kila siku.
Aidha
ameongeza kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya sensa ya
watu na makazi hali ya kuwa yamebaki masaa machache kufikia zoezi hilo lakini
kuna baadhi ya watu bado hawajaelimika.
Taarifa
iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ilieleza kuwa Rais Samia Suluhu
Hassan ameridhia siku ya Jumanne Agosti 23 kuwa ya mapumziko na watu wote wanatakiwa
kubaki nyumbani kwaajili ya kuhesabiwa.
0 Comments