RAIS
wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu amewataka maafisa wa
uhamiaji nchini kubuni mbinu mbalimbali za kiteknolojia ili kuweza kukabiliana
na mbinu mpya za uhalifu zinazojitokeza mara kwa mara.
Ameyasema
hayo leo katika ziara ya kufunga mafunzo ya awali ya askari wa Uhamiaji Jijini
Tanga ambapo amewataka maafisa wa jeshi la uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na kufuata
Sheria na taratibu zilizopo nchini.
Rais
Samia amesema kwa kufanya hivyo wataweza kuviwezesha vyombo vya usalama kutekeleza
vyema majukumu yake ya ulinzi wa Taifa.
Nimesikia kuna baadhi ya maafisa na maskari wasio waaminifu na kuna kesi katika mafaili kwenye fedha zinazotoka za vibali wanazigeuza za kwao na kuweka mifukoni
Amesema
katika utafiti mdogo uliofanywa mwaka huu hususani kwenye vituo vya Zanzibar
pamoja na Dar-saalam wamegundua upotevu mkubwa wa fedha za viza ambao unafanywa
na maafisa wa uhamiaji.
Aidha
Rais Samia ameagiza maafisa hao kushughulikiwa ili iwe fundisho kwa wengine na
kurudi katika maadili.
0 Comments