JESHI
la Zimamoto na Ukoaji limefanya mabadiliko ya tozo za ukaguzi wa usalama dhidi
ya majanga ya moto katika majengo na maeneo mbalimbali pamoja na utaratibu wa ukusanyaji
tozo ili kuleta tija na kuliwezesha Jeshi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi
zaidi.
Awali
Jeshi lilibeba jukumu la kumfata mteja na kuomba kufanya ukaguzi katika jengo,
eneo au chombo cha usafiri ambapo kwa sasa umeonekana kuboreshwa zaidi.
Hayo
yamesemwa Leo jijini Dodoma na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto,
Puyo Nzalayamisi na kuwataka wateja au wamiliki wa majengo, eneo au chombo cha
usafiri ambaye hajafanyiwa ukaguzi kufika ofisi za jeshi na kuomba kukaguliwa
wakati bado wakiendelea kuboresha mifumo yao ili wateja waweze kuomba kupitia
mitandao.
Amesema
baadhi ya tozo zimefutwa kama vile mashamba ya kahawa, mikonge pamoja na chai
lakini pamoja na kushuka kwa gharama hizo bado kuna maingizo mapya ya tozo
ikiwa ni sehemu ya karakana, vituo vya usafirishaji na wafanyabiashara ya kufua
nguo 'dry cleaner'.
Tunaendelea kuwasihi wamiliki wa majengo, maeneo pamoja na vyombo vya usafiri kufuatilia taarifa zetu kupata elimu, Sheria na nyaraka zingine kupitia mitandao yetu ya kijamii (Instagram @tanzimamoto, Twitter @tanzimamoto, Facebook @ Jeshi la zimamoto na ukoaji) na kuendelea kuwasiliana nasi kupitia namba zilizoainishwa kwa changamoto zote kuhusu mabadiliko haya
Aidha
ameendelea kuwakumbusha wananchi kushiriki katika zoezi la sensa litakayofanyika
Agosti 23 mwaka huu kwa maendeleo ya taifa kutokana na kuwasaidia katika zoezi
la upangaji wa vitendea kazi pamoja na upangaji wa rasilimali watu katika vituo
vyao vya kazi.
0 Comments