📌SALMA HAROUN & JOSEPHINE MTWEVE
JAMII imetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwajali
na kuwawezesha watu wenye ulemavu kwa kushirikiana katika shughuli mbalimbali
za kijamii kwa lengo la kujenga umoja na kuwafanya wajihisi wana nafasi ya
kushiriki vitu mbalimbali kama watu wengine.
Mwita Marwa ambaye ni mlemavu wa miguu lakini pia ni
fundi mkuu katika Karakana ya watu wenye ulemavu Dodoma (KAWADO) inayohusika na
utengenezaji wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ameishauri jamii
iwakumbuke na kuwajali watu hao.
Marwa ameiomba serikali kwa kushirikiana na Taasisi na
Makampuni iwawezeshe watu wenye ulemavu kwa kuwapa mitaji na kuendeleza vipaji
vyao kwa kuwasomesha vyuo vinavyohusika na fani mbalimbali ili kuwaepusha na
suala la utegemezi kwa watu wengine.
Mimi hapa natengeneza vifaa vya kuwasaidia walemavu lakini pia sijaajiri watu ila nina vijana ninaosaidiana nao kazi lakini pia nafundisha watu wengine wenye ulemavu kama mimi ambao wengine mpaka sasa tayari wamefungua ofisi zao sehemu nyingine na zinawasaidia kuendesha maisha yao
Marwa.
Aidha Marwa amewataka walemavu kubadilika na
kuhakikisha wanajikita katika shughuli za kijamii kama biashara kwa kuomba
mitaji kwa watu wenye uwezo katika jamii kwa lengo la kuepuka utegemezi kwa
watu wengine.
"Mimi sikusomeshwa na wazazi wangu ila nilijisomesha mwenyewe elimu ya shule ya msingi lakini nikapata msaada wa kwenda chuo cha ufundi na mpaka sasa mimi ndo msaada kwa wazazi wangu na kwa watu wengine wenye ulemavu
Marwa.
Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi katika karakana
hiyo Michael amesema kutokana na upeo mdogo wa watu wanaona watu wenye ulemavu
hawana msaada katika jamii lakini Marwa ni moja kati ya walemavu waliothubutu
kuonyesha uwezo wake katika jamii.
Amesema jamii inatakiwa kuwachukulia watu wenye
ulemavu kuwa kama watu wengine ambao wanauwezo wa kufanya kazi kutokana na wote
kuwa na haki sawa katika kujumuika na kushiriki mambo mbalimbali ya kijamii.
0 Comments