📌RHODA SIMBA
SHIRIKA la Foundation for Civil Society (FCS) limetoa ruzuku ya Shilingi 3,957,301,580 sawa na Bilioni nne (4) kwa Asasi za Kiraia (AZAKI) 89 Tanzania bara na visiwani kutekeleza miradi ya kimaendeleo chini ya programu za utawala bora katika sekta za maji, elimu, afya na kilimo; usawa wa kijinsia; ujumuishwaji wa vijana na watu wenye ulemavu, na ujenzi wa amani na mshikamamo wa kijamii kwa mwaka 2022-2023.
Akizungumza Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) Francis Kiwanga amesema kuwa taasisi zilizoomba zilikuwa zaidi ya 1200 kutoka Tanzania nzima lakini taasisi zilizofanikiwa ni 89 hivyo hizo fedha zimegawanywa kwenye mikoa yote na wadau wote ambao tunafanya kazi nao kwa mwaka huu.
Amesema kuwa wametoa ruzuku kiasi cha bil.4 kwa mwaka huu na wadau wote watafanya kazi kwa mwaka huu 2022 na mwakani 2023, hivyo wameweza kupata wadau 86 wanaotoka katika mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani, ambao watakuwa wanafanya kazi kusukuma agenda ya utawala bora nchini.
Lakini pia utawala bora katika maswala ya kuleta usawa wa kijinsia, kufatilia rasilimali katika sekta ya maji, elimu, afya na kilimo na kufanya kazi na watu wa makundi maalum,kupiga vita juu ya ukatili wa kijinsia ,lakini pia kundi la vijana kuhakikisha rasilimali zinazotolewa na serikali na wadau wengine basi ziwe zinawafikia watu hao
Amesema kuwa eneo lingine wanalolifanyia kazi ni eneo la kutunza amani na utatuzi wa migogoro Tanzania bara na Visiwani
Tunafahamu kwa sasa kumekuwa na ongezeko la migogoro kwenye rasilimali kama tunavyoona sehemu nyingine za wakulima na wafugaji wamekuwa na migogoro. Hivyo basi kuna taasisi zaidi ya 10 ambazo zitakuwa zinafanya kazi katika utatuzi wa migogoro hapa nchini.
Lakini pia serikali ina mipango mingi sana na inapeleka rasilimali nyingi katika sekta ya kilimo hivyo sisi wajibu wetu ni kuhakikisha je rasilimali hizo zinawafikia walengwa, hivyo kupitia taasisi ambazo tumezichagua mwaka huu tutahakikisha eneo la kilimo kuna ushirikishwaji mzuri wa wananchi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Women for Initiative Benadeta Choma amesema kuwa Ruzuku zinazotolewa na serikali na wafadhili zinawasaidia kujenga uelewa wa wananchi na hasa katika sekta ya afya ambapo wanaenda kuboresha afya ya wana jamii kwa Wilaya ya Nkinga.
0 Comments