DKT.GWAJIMA ATOA PONGEZI KWA MALEZI YANAYOFANYWA NA TAASISI YA WATOTO YATIMA YA KIJIJI CHA MATUMAINI.

 ðŸ“ŒJOSEPHINE MTWEVE & SALMA HAROUN

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima amewapongeza walezi kwa maono ya uangalizi kwa watoto kwa mfumo wa kifamilia unaofanyika katika Taasisi ya kulelea watoto yatima ya kijiji cha matumaini.

Ni katika maadhimisho ya Jubilee ya miaka ishirini ya Taasisi ya kulelea watoto yatima ya Kijiji cha Matumaini Jijini Dodoma kinachojihusisha na malezi ya watoto wanaotoka katika mazingira hatarishi wakiwemo waliopoteza wazazi wao ambapo amesema mwaka jana mwishoni wameweza kuzindua mpango kazi wa taifa wa malezi na makuzi ambapo wanajenga vituo vingi vya makuzi na malezi.

Amesema Taasisi hiyo ya kijiji cha Matumaini imeweza kujipanga vyema katika mifumo yote inayoweza kujibu mahitaji ya makuzi ya watoto katika suala zima la kujifunza.

Serikali ipo pamoja nanyi wakati wowote mtakapohitaji ushirikiano, hata huu ujenzi unaoendelea hatutawaacha peke yenu tutakua pamoja kutafuta fursa za rasilimali mbalimbali kwaajili ya kuendeleza

Aidha Dkt. Gwajima amewaagiza wamiliki na waendeshaji wa makao yote nchini kuhakikisha kila mtoto anayepokelewa anaandaliwa mpango wa huduma unaojumuisha mpango wa kutoka makaoni na taarifa zote zihifadhiwe katika jalada la mtoto.

Kwa upande wake msimamizi wa utawala katika kijiji cha Matumaini Baltazar Sungi ameiomba Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu kuwasaidia kuongea na Wizara ya Fedha ili kupata tamko rasmi la utambuzi kutoka kwa kamishna wa Mamlaka ya mapato kuwa kijiji cha Matumaini ni shirika linalotoa huduma za hisani.

Amesema kuna haja ya kupanua shule ya sekondari kwa kuongeza madarasa na maabara vilevile mabweni kwaajili ya watoto wa shule za msingi.



 

Post a Comment

0 Comments