AUWSA: TUMEFANIKIWA KUONGEZA UPATIKANAJI WA MAJI KUTOKA ASILIMIA 66.8 HADI ASILIMIA 75

 

📌RHODA SIMBA

KUTOKANA na juhudi mbalimbali zinazoendelea kufanyika ili kuboresha huduma ya Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha na miji midogo ya Longido, Usa River, Monduli na Ngaramtoni, Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) imefanikiwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji safi kutoka asilimia 66.8 kwa mwaka 2020/21 hadi asilimia 75 mwaka 2021/22.

Akizungumza hii leo jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Justine Rujomba amesema wanaendelea kuongeza mtandao katika utoaji huduma hadi kufikia asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2025.

Mamlaka imeweza kuongeza upatikanaji wa huduma za maji safi kutoka asilimia 66.8 ya wakazi wa Jiji la Arusha mwaka 2020/21 hadi asilimia 75 mwaka 2021/22 na wateja waliounganishiwa huduma ya maji wameongezeka kutoka wateja 71,183 Juni 2021 hadi wateja 95,748 Juni 2022, 
 Mamlaka inaendelea kuongeza mtandao katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma ili kuweza kufika malengo ya ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kufikia asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2025. AUWSA imefanikiwa kutumia mfumo wa GIS kutunza kumbukumbu ya mtandao wote wa maji pamoja na maunganisho ya wateja ili kurahisisha utambuzi wa mtandao

Rujomba

Aidha Mhandisi Rujomba amesema AUWSA inaendelea kupambana na upotevu wa maji kwa kutoa elimu juu ya utunzaji wa miundombinu ya majisafi na kuepukana na wizi wa maji kwa kutoa taarifa ya wizi pamoja na uharibifu wa miundombinu ya maji safi kupitia kituo cha huduma kwa wateja na kuongeza kuwa hadi sasa zaidi ya watu 55 wamekamatwa kwa wizi wa maji na wamelipa faini ya kiasi cha shilingi milioni 65.

Kujenga chemba za kuhifadhia dira za wateja dhidi ya uharibifu na wizi wa dira za maji, ambapo chemba 1,237 zinajengwa ili kuhamishia dira 5000 za wateja wa majumbani,

Amesema AUWSA inaendelea kupambana na upotevu wa maji kwa kutoa elimu juu ya utunzaji wa miundombinu ya majisafi na kuepukana na wizi wa maji kwa kutoa taarifa ya wizi pamoja na uharibifu wa miundombinu ya majisafi kupitia kituo cha huduma kwa wateja.’’ amesema Rujomba

Kuhusu vipaumbele vya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 amesema mamlaka hiyo inatekeleza mradi mkubwa unaoendelea ili kuongeza hali ya upatikanaji wa maji safi kutoka asilimia 75 ya sasa hadi asilimia 100 ya wakazi wa Jiji la Arusha mwaka 2023.

Kuendelea kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira katika miji midogo ya Monduli, Ngaramtoni, Usa River na Longido, kutenga fedha kwa ajili ya stahili za watumishi, kutenga fedha kwa ajili ya malipo ya watoa huduma mbalimbali wanaoshirikiana na mamlaka kuendelea kujiunga na kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA ya serikali kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma na kupunguza gharama kwa serikali kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa miundombinu ya majisafi na usafi wa mazingira.

Rujomba

Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) ni Taasisi ya Serikali inayofanya kazi zake chini ya Wizara ya Maji. Mamlaka hii ilianza kufanya kazi Julai 1, 1998 baada ya kuanzishwa kwa sheria ya maji ya mwaka 1997 iliyobadilishwa na sheria ya maji safi na usafi wa mazingira na. 5 ya mwaka 2019 ikiwa na majukumu ya kuhakikisha inatoa huduma bora za maji safi na uondoaji wa majitaka kwa ufanisi na kwa uhakika kwa kutumia rasilimali na teknolojia iliyopo kwa maendeleo endelevu ya Jiji la Arusha na Tanzania kwa ujumla.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments