UTPC YATOA JAKETI KULINDA WAANDISHI MAHALA PA KAZI

 

📌SAIDA ISSA

MUUNGANO wa Club za Waandishi wa Habari Tanzania UTPC imetoa Safety Jaketi 25 kwa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma kwa lengo la ulinzi na usalama wawapo mahala pa kazi.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Ulinzi na Usalama kwa waandishi kutoka mikoa tofauti tofauti yaliyofanyika jijini hapa rais wa UTPC Deo Nsokolo alisema muhimu kuhakikisha waandishi wanalinda usalama wanapokuwa katika kazi zao.

Usalama ni jambo la kwanza na la muhimu hasa uwapo kazini hivyo UTPC kwa kutambua umuhimu wa wanahabari tumeona ni vyema kutengeneza hizi jaketi maalumu kwa waandishi Tanzania nzima lakini kwa kuwa tuko Dodoma watawakilisha kupokea na mikoa mingine jaketi hizi zitawakuta huko huko

Nsokolo.

Aidha alisema kuwa ni muhimu mwanahabari kutambua hali ya hatari kabla ya kufika mahala pa kazi na namna ya kukabiliana nayo kwani kundi la wanahabari liko katika hatari muda wote kutokana na kazi.

Alisema UTPC kwa kushirikiana na wafadhili mbalimbali itaendelea kutoa elimu na mafunzo kwa waandishi wa habari ili kuweza kuwajengea uelewa juu ya ulinzi na usalama.

Akizungumza baaada ya kupokea jaketi hizo mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dodoma, Mussa Yusuph aliishukuru UTPC kwa kutambua umuhimu wa waandishi wa habari na kuwapatia jaketi hizo.

Kwa niaba ya wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari Dodoma tunashukuru sana uongozi wa UTPC kuhakiksha mnatambua thamani ya waandishi wa habari na kuweza kuandaa jaketi maalumu ikiwa na lengo la kumfanya mwanahabari aweze kujiamini awapo katika kazi

Mussa.


Kwa upande wake Mtaalamu wa mawasiliano ya umma Dkt.Joyce Bazira ambaye alikuwa akiwapatia mafunzo wanahabari alisema kuwa muhimu kila mwandishi kutambua kuwa hakuna story nzuri kuliko maisha yake.

Mnapokuwa katika majukumu yenu mhakikishe mnatambua kuwa hakuna story nzuri zaidi ya maisha yako, mkiwa katika majukumu yenu suala muhimu ni kuhakikiksha mnatambua ulinzi na usalama katika mazingira yenu ya kazi

Bazira

Mafunzo ya Ulinzi na Usalama mahala pa kazi yalifanyika jijini Dodoma kwa kuandaliwa na UTPC kupitia wafadhili washirika la International Media Support{IMS}linalopewa fedha kutoka umoja wa Ulaya{EU}.



Post a Comment

0 Comments