SIMBAYA MKURUGENZI MTENDAJI MPYA UTPC

 


📌MWANDISHI WETU 

Taarifa iliyotolewa na Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo akiendelea na vikao vya mazungumzo ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTPC na wafadhili SIDA amemtaja Mkurugenzi mpya kuwa ni Kenneth Simbaya ambaye aliwahi kuiongoza UTPC siku za nyuma.

Nikiwa rais wa UTPC nina furaha kutangaza kuwa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania imepata Mkurugenzi Mtendaji mpya Ndg. Kenneth Simbaya amechukua nafasi ya Abubakar Karsan ambaye amestaafu 

Nsokolo

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) inampongeza Ndg. Kenneth Simbaya kwa kuaminiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya UTPC kushika wadhifa huo lakini pia Ndg. Karsan kwa utumishi wake uliotukuka kwa UTPC inayowaunganisha wanahabari wote Tanzania kwa lengo la kukuza weledi na kuimarisha ustawi wa tasnia ya Habari nchini.

Post a Comment

0 Comments