📌RHODA SIMBA
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesaini mkataba wa maridhiano baina ya Wizara na Kampuni ya EXNTENSIA ya Nchini Uingereza wenye lengo la kuandaa kongamano la TEHAMA na ubunifu hapa nchini .
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo leo Julai 25 jijini Dodoma Katibu Mkuu Kutoka Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi amesema kongamano hilo litasaidia kuchangia uchumi wa kidigitali na litawaleta wadau mbalimbali wenye nia ya kuwekeza katika TEHAMA
Wadau watakuja kujifunza nchini kwetu na kongamano hilo tunatarajia kufanyia September 7 na 8 na linatarajiwa kuwa na wageni takribani 300 watakaokuja kujifunza na hawa watakuja kukutana na wananchi wenye nia ya kuwekeza katika TEHAMA na tunatarajia kuwa na aina nyingi ya watu waliobobea katika sekta hiyo
Dkt Yonazi
Aidha Dk Yonazi amesema kuwa Tanzania ina mpango wa kuwa nchi yenye kitovu Cha TEHAMA na ubunifu katika Eneo la nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa kuwa Tanzania ni nchi inayounganisha mkongo wa Taifa.
Nae Mkurugenzi kutoka idara ya TEHAMA Mulengwa Mnakwa amesema kongamano hilo litafanyika tarehe 7 na 8 Septemba Jijini Dar es salaam na wanategemea kuwa na washiriki 300 Kutoka ndani na nje ya nchi.
Vile vile kongamano hilo litahudhuriwa na mashirika makubwa ikiwemo shirika linalosimamia mawasiliano duniani litakuwepo na wale wanaosimamia mawasiliano Afrika watakuwepo na sisi itakuwa kama ni fursa kwa watanzania kuweza kuwekeza hapa nchini kwa lengo la kuongeza ajira hapa nchini
Mnakwa
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa Mkongo wa Taifa ni nguzo muhimu Katika kujenga uchumi wa kidigitali.Uwekezaji huu unatukutanisha na wadau mbalimbali kwani Uchumi kidigitali ni nyezo muhimu unatukutanisha na wadau mbalimbali na watu ambao wanaweza kuongeza uwekezaji hapa nchini”
Msigwa
0 Comments