📌RHODA SIMBA
MKUU wa Mkoa wa
Dodoma Anthon Mtaka ametoa siku 10 kwa wakurugenzi wa Halmashauri za
Dodoma kukutana na kupitia taarifa za upokeaji,utoaji na uzambazaji
wa dawa katika Wilaya zao.
Kadhalika amewataka
wakurugenzi hao kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi ambao watabainika
kuhusika na upotevu au upungufu wa dawa katika Zahanati, Vituo vya afya na
Hosptali za wilaya na Mkoa.
Mtaka ameyasema hayo
leo Julai 20 Jijini hapa wakati wa kikao chake na viongozi wa Wilaya katika
sekta ya afya, kwa ajili kupitia taarifa ya upokeaji,utoaji na usambazaji wa
dawa.
Hizi siku 10 tunazopeana ziwe za kazi ambazo lengo lake ni kufanya ukaguzi na kujiridhisha kwa dhati kuhusu matokeo ya dawa kwenye Vituo vya afya, Zahanati na Hospitali za Wilaya na Mkoa. Baada ya hapo kutakuwa na kikao cha kupokea taarifa na pale ambapo kutabainika mapungufu wakurugenzi wanayo nafasi ya kuchukua hatua za kinidhamu.
Ameongeza kuwa
Tutakaa kikao kingine cha kupokea taarifa ya ukaguzi wa Vituo vya afya, Zahanati, Hospitali za Wilaya na Mkoa kwa asilimia 100 katika upokeaji,utoaji na usambazaji wa dawa na baada ya hapo Katibu Tawala wa Mkoa ataweza kuchukua hatua kwenye maeneo ambayo yameonyesha upungufu
Amesema taarifa
itakayotolewa na Wakurugenzi ionyeshe dawa kiasi gani zimepokelewa,thamani ya
dawa, thamani ya upungufu na upotevu ili waweze kulinganisha madawa tuliyopokea
toka serikali kuu na wadau wengine ili tuweze kufanya ulinganisho na kubaini
kama tuko salama ili tufanye maamuzi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kongwa amesema kikao hicho ni muhimu kutokana
na serikali kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.
Amesema maelekezo yaliyotolewa
na Mkuu wa Mkoa wameyachukua na wanaenda kufanyia kazi na kuhakikisha siku 10
alizotoa wanaenda kupitia taarifa na kuchukua hatua kama walivyoagizwa.
Kikao kimeenda vizuri na sisi tukiwa kama wasimamizi wakuu wa fedha katika ngazi ya Wilaya tutahakikisha tunapitia taarifa kama tulivyoagizwa na pale ambapo tutaona kuna haja ya kuchukua hatua hatutasita kufanya hivyo
0 Comments