RAIS SAMIA AWATAKA MADEREVA BODABODA KUEPUKA VITENDO VYA UPORAJI

 

📌RHODA SIMBA

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka waendesha bodaboda na bajaji nchini kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika zoezi la sensa huku akiwataka kulinda hadhi ya kazi zao kwa kuepuka kashfa ya vitendo vya uporaji na ujambazi kwani sekta ya usafirishaji ni muhimu kwa wananchi.

Rais Samia ameyasema hayo Leo Julai 24 Jijini Dodoma kwa njia ya simu katika Kongamano la kuimarisha ushiriki wa waendesha Bodaboda na bajaji katika sensa ya watu na makazi ambapo amesema kuwa yuko tayari kutatua changamoto za madereva Bodaboda ili walinde heshima yao.

Aidha Rais Samia amesema Serikali haitawaacha nyuma madereva hao na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kusikiliza changamoto zao zinazowakabili ili aweze kuzitatua mara moja.

Ninyi ni watu muhimu sana katika Taifa letu kuna baadhi yenu wanawaharibia sifa niwasihi msikubali kuharibiwa sifa na baadhi yenu ambao wanatumia usafiri huo kwa kupora,kukaba na kutumika katika ujambazi

Elezeni changamoto zenu zote Mkuu wa Mkoa ataniletea na mimi nimeahidi kuzitekeleza changamoto zenu ikiwa ninyi ni sekta muhimu kwa wananchi wa hali ya chini kutokana na huduma mnayoitoa

Rais Samia.

Akizungumza mara baada ya kupokea simu ya Rais Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema kuwa wao kama viongozi wa Mkoa wako tayari kusikiliza kero za madereva hao na kuhakikisha zinamfikia Rais Samia kama alivyo ahidi.

Mheshimiwa Rais tunashukuru sana kwa kuona umuhimu wa Kongamano hili na kuamua kuongea na madereva hawa, Mimi pamoja na viongozi wenzangu tupo hapa kwaajili ya kuhakikisha kila Dereva aliyefika hapa anaeleza changamoto zake

Madereva hawa ni kutoka mikoa mbalimbali na wao kuwatambua umuhimu wa Kongamano hili wametuma wawakilishi wakila Mkoa ili waweze kuja kueleza kero zinazowakabili na nawaahidi kuwa tunawasikiliza na zitakufikia mezani kwako,"amesema Mtaka.

Kwa upande wake dereva bodaboda Mkulia Seif akitoa kero yake katika amesema gharama ya leseni kwa bodaboda na bajaji iko sawa na ya magari makubwa ambayo ni elfu 70 hivyo ameiomba Serikali iwapunguzie gharama.

Naye Jackson Juma Dereva Bodaboda ameiomba Serikali kuangalia suala la faini kwa upande wao kwani Mheshimiwa Rais alipunguza kutoka elfu 30 mpaka kufikia elfu 10 na kuiomba Serikali kuzingatia agizo hilo lisimamiwe.

 

Post a Comment

0 Comments