NDALICHAKO AKUTANA NA WASTAAFU KUJADILI CHANGAMOTO

 

📌RHODA SIMBA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kuanza kusikikiza changamoto za wastaafu huku akibainisha kuwa changamoto  kubwa aliyokutana nayo kwa wastaafu hao ni uelewa mdogo na kuahidi kuzitatua.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya kupokea malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wastaafu juu ya mafao yao huku akisema malalamiko aliyokutana nayo mengine ni kutokana na kukosa elimu na akatoa rai kwa watendaji kuhakikisha wanafungua milango kwa kuwasikiliza wastaafu na kutatua changamoto zao.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma a mara baada ya kuwasikiliza baadhi ya wastaafu hao amesema kuwa ameona ni vyema kukutana na wastaafu hao na kujua changamoto zinazowakabili ili kuweza kuzitatua ambapo aliambatana na watendaji wakuu wa mifuko na wataalamu .

Zile changamoto za kutatua papo kwa papo tunazitatua moja kwa moja na zile changamoto zinahitaji muda kufuatiliwa tunachukua vielelezo kwaajili ya kufanyia kazi ambapo nimeweza kuwaona na kuongea nao wastaafu 10 katika hao wastaafu 2 changamoto zao zimesha tatuliwa kwani ilikuwa ni ufafanuzi nawao walikuwa hawana uelewa  

Prof Ndalichako.

Aidha amesema zoezi la kusikiliza wastaafu litaendekea kufanyika katika Mikoa mingine wastaafu wa NSSF na PSSSF na atatatua changamoto zao moja kwa moja na changamoto zinazohusu Hazina zitatatuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Kwa upande wao wastaafu hao walimpongeza Waziri huyo mwenye dhamana kwa kuweza kutenga siku na kukaa na kusikikiza kero za wastaafu.

Akiongea na wanahabari kwa niaba ya wastaafu wenzake Ramadhan Abdallah msaafu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara Geleza la Msalato Dodoma alisema baada ya kufika hapo walipokelewa na kutatuliwa kero zao vizuri na vinyongo vyoa kuondoka.

Mimi nilifika hapa baada ya kupata tangazo kwenye mitandao kuwa Waziri mwenye dhamana Ndalichako atakutana na wastaafu na kero yangu nilikuwa nahisi napunjwa mafao yangu lakini baada kufika hapa na kukutana na wataalamu na kunikokotolea mafao nimejilidhisha mafao yangu yalikuwa sawasawa na kero yangu imeisha, .

 

Post a Comment

0 Comments