📌MJJWM
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amewataka waandishi wa habari kuelemisha
jamii kuhusu Programu ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya
Mtoto na umuhimu wa kutoa Malezi Bora ndani ya kipindi cha Umri miaka 0 hadi 8.
Dkt. Gwajima
ameyasema hayo jijini Dodoma Julai 4, 2022 wakati akifungua Mafunzo ya Kitaifa
ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ambapo jumla ya
Washiriki 79 kutoka Mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wanapatiwa Mafunzo ya
siku sita.
Dkt. Gwajima amesema kuwa kwakuwa Mafunzo hayo
yanawashirikisha na watu wa Kada zingine ambao ni Maafisa Ustawi na Maendeleo
ya Jamii lakini pia kutoka Asasi za kiraia ni imani yake kuwa tija
iliyokusudiwa itapatikana wakishirikiana.
Ameongeza kuwa Waaandishi wa Habari ni kada muhimu
sana katika kusukuma Ajenda za Maendeleo ya Makuzi na Maendeleo ya Mtoto, hivyo
wakitumia kalamu zao vizuri wataweza kuinua taaluma zao lakini watasomeke vema
kwa Taifa kwa uzalendo wao.
Lingine lakufurahisha ni kuwa Mafunzo haya yamehusisha pande hizi mbili za Muungano lakini ifahamike mwingiliano wetu na kutembeleana Mara kwa Mara kati ya pande mbili hizi itachochea na kuimarisha zaidi Muungano wetu, kitu ambacho hata Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amekuwa akikisisitiza
Waziri Gwajima.
Kwa Upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum ambaye ni Mkurugenzi wa
Watoto, Sebastian Kitiku alisema Elimu kwa Kada hizo ni Mwanzo wa kuzifikia
kada zingine ili ziweze kushiriki kawamakribu katika kuhakikisha jamii inapata
uelewe wa namna ya kuwaoatoa Watoto malezi bora kupitia Programu hiyo
Mhe. Waziri Elimu hii ambayo inatolewa kwa muda wa siku sita ni mwanzo tu lakini Shabaha yetu nikuwafikia watu wa Kada zote nchi nzima kwakuwatumia Maafisa Ustawi na Maendeleo ambao wamepata elimu hiiKitiku.
Akitoa Maelezo kuhusu Mafunzo hayo Mkurugenzi Mkaazi
Craig Ferla kutoka taasisi ya Crossfire alisema muelekeo ni kuandaa Kadi ya
kujipima kwa kila mmoja ili kuona kama wanapiga hatua kutokana na elimu
inayotolewa na lengo likilokusudiwa.
Mhe. Waziri utakumbuka ulipo muwakilisha Mhe. Rais wakati wa uzinduzi wa Program hii uliagiza suala la Score Card leo tunaomba tukuhakikishie kuwa suala lile tumelizingatia hivyo katika utendaji wetu tumeona tuwe nalo
Craig.
0 Comments