MGANGA MKUU WA SERIKALI ATOA TAARIFA KUHUSU UGONJWA USIOFAHAMIKA.

 

📌RHODA SIMBA

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe hii leo ametoa taarifa kuhusu ugonjwa usiofahamika Mkoa wa Lindi ambapo amesema kuwa kufuatia kuripotiwa kwa ugonjwa huo mpaka sasa watu watatu wamefariki na Wizara iliunda tume ya wataalam huku sampuli za awali zilizopimwa katika maabara ya taifa zikionesha majibu hasi kwa ugonjwa wa Ebola, Marburg na UVIKO-19.

Akitoa taarifa hiyo hii leo jijini Dodoma Dkt. Sichalwe amesema kuwa hadi kufikia tarehe 12 Julai kulikuwa na jumla ya wagonjwa 11, kati yao watatu (3) wamefariki na wagonjwa wawili waliokuwa wametengwa katika kituo cha afya Mbekenyera, wamepona na kuruhisiwa kurudi majumbani mwao.

Baada ya kupata taarifa hiyo Wizara ya Afya iliunda timu ya wataalamu kutoka katika idara ya magonjwa ya dharula na majanga idara ya kinga Mkemia Mkuu wa serikali na kuongeza timu ya watafiti kutoka taasisi ya utafiti NIMR na timu ya Afya ya Halmasahuri ya Ruangwa

Dkt.Sichwale

Aidha ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutafuta watu wengine wenye dalili za ugonjwa huo ambazo ni dalili za homa, kuvuja damu (hususani puani), kichwa kuuma na mwili kuchoka sana ili kuwatambua mapema na kuwatenga ili kuzuia ugonjwa usisambae

Tunaendelea kufuatilia watu ambao walitengamana nao ndani ya siku 21 na kuhakikisha kwamba ndani ya siku hizo wanapata huduma pia tunaendelea kutoa huduma na kwa wale ambao wamepata ugonjwa huo tunawaambia waendelee kujitenga ili wasiwaambukize wengine

Dkt Sichwale

Mnamo tarehe 7/7/2022, Wizara ya Afya ilipokea taarifa toka kwa Mganga Mkuu Mkoa wa Lindi kuwa katika Halmashauri ya Ruangwa kumekuwepo na ugonjwa usio wa kawaida kutoka kituo cha afya Mbekenyera hivyo Wizara inatoa wito kwa wananchi kuwa watulivu wakati ikiendelea kulifanyia kazi suala hilo sambamba na kutoa wito kwa wananchi kutumia vituo vya kutolea huduma za afya pale wanapojisikia kuumwa.

 

Post a Comment

0 Comments