📌RHODA SIMBA
SERIKALI imesema imewekeza kwa kiasi kikubwa katika miradi ya kuboresha miundombinu ikiwemo reli na barabara ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kibiashara,kupunguza misongamano mijini na kuvutia uwekezaji.
Hayo yamesemwa leo Julai 26 Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti usafiri ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuhakikisha inaboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo reli na barabara ili kuhakikisha miji inakuwa katika mipangilio mizuri na kuvutia.
Aidha amesema kuwa Mamlaka imejiwekea mpango mkakati wa miaka mitano, (2020/21- 2024/25), wenye malengo ambayo ni kuimarisha programu za kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza katika sekta ya usafirishaji ikiwemo VVU/ UKIMWI, Kuimarisha mkakati wa kitaifa dhidi ya Rushwa na mpango wa utekelezaji, Kuimarisha uwezo wa Mamlaka kutekeleza majukumu ya kiudhibiti, Kukuza ushindani na ufanisi katika sekta ya usafirishaji,
Kuboresha uwezo wa kusimamia usalama wa usafiri ardhini,kuboresha mazingira endelevu katika usafiri ardhini na,kukuza huduma bora za usafiri ardhini ili kutekeleza malengo haya ipasavyo,
Mamlaka imejipanga
kuwafikia wananchi kupitia ofisi zake zilizopo mikoa yote Tanzania bara na
kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA inayorahisisha utoaji wa huduma katika
sekta zinazodhibitiwa.
Amesema mamlaka imepanga kutoa mafunzo kazini kwa Wafanyakazi Muhimu wa Usalama katika undeshaji wa reli (Safety Critical Workers) kwa TAZARA na TRC ili kuwaongezea ujuzi wa kutimiza majukumu yao kwa weledi.
Mafunzo ya aina hii husaidia kuwafanya wafanyakazi hao muhimu kuzuia ajali zitokanazo na makosa ya kibinadam (Human Error, Tathmini inaonesha kwamba, makosa ya kibinadamu katika uendeshaji wa shughuli za reli huchangia asilimia zaidi ya 85% ya ajali za treni kwa TRC na TAZARA
Ameeleza kuwa kwa kuendesha mafunzo hayo kutatatua kwa kiasi kikubwa ajali zitokanazo na makosa ya kibinadamu, LATRA imepanga kuandaa kanuni za kutunza mazingira katika undeshaji wa reli.
Ifahamike kwamba maeneo mengi ya ushoroba wa reli hasa miji yamesongwa na makazi ya watu ambao kwa kiasi kikubwa wamekaribia sana eneo la undeshaji wa reli, Kupitia kanuni hizo, maboresho yatafanyika kwa kuwashirikisha wadau muhimu wakiwemo wananchi na serikali zao za vitongoji/mitaa, namna bora ya kuhifadhi ushoroba wa reli bila kuharibu miundombinu
Amesema kanuni hizo zitakuwa shirikishi kwa wadau wote wanaohusika, Mamlaka itahakikisha usalama wa treni za mjini (Commuter Trains) unaimarishwa, hasa katika jiji la Dar es Salaam, ambapo TAZARA na TRC zinaendelea kutoa huduma ya usafiri huo.
Mpango mkakati ni kuwa treni hizi za mjini zinaendeshwa kwa maboresho makubwa ikiwemo ubora wa siti, vitasa vya milango, vishikizi kwa abiria na taa za ndani ya mabehewa.
Uwepo wa treni za mjini (Commuter) husaidia kupunguza msongamano kwenye mabasi ya daladala, Kwa mujibu wa Kifungu cha 5(g) cha Sheria ya LATRA Na. 3 ya mwaka 2019,Mamlaka itaendelea kuishauri serikali namna bora ya uendeshaji wa reli kwa njia iliyo salama na kuufanya usafiri wa reli kuwa wa kuaminikaAidha LATRA imepanga kuendesha semina mbalimbali kwa wananchi na wadau wanaotumia reli ili kuongeza uelewa wa usalama, Hili ni takwa la kisheria kama linavyoainishwa katika Kifungu cha 6(f) cha Sheria ya LATRA Na. 3 ya mwaka 2019.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ilianzishwa kwa Sheria Na. 3 ya Mwaka 2019 ili kudhibiti huduma za usafiri ardhini katika sekta za reli na barabara. Sheria ya LATRA ilifuta Sheria Na. 9 ya mwaka 2001 iliyoanzisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).
0 Comments