📌RHODA SIMBA
CHAMA Cha Wakandarasi Wazawa (ACCT) kimeandaa kongamano maalumu la wakandarasi Wazawa kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia kwa kutwaa tuzo na kuifanya Tanzania kutambulika Kimataifa.
Kadhalika kimesema Rais Samia Suluhu Hassan alistahiri kupewa tuzo ya heshima ya Babacar ya mwaka 2022 kwani serikali yake imepata mafanikio katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Hayo yamesemwa Leo Juni 3 jijini hapa na Mwenyekiti wa ACCT Thobias Kyando wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano lililoandaliwa na wakandarasi wazawa kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia.
Rais Samia alistahili kabisa kupewa tuzo hii ya heshima kwasababu amefanya mambo makubwa katika sekta ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, barabara, na bandari ndio maana akaibuka kidedea wa tuzo hiyo na sisi tukiwa wadau wa miundombinu tunampongeza sana
Amesema ujenzi wa miundombinu imekuwa na faida hasa kwa wandarasi Wazawa kwasababu wanahusika moja kwa moja kuiboresha pindi wakandarasi wageni wanapoondoka.
Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kuendelea kuwaamini wakandarasi wazawa kwa kuwapatia tenda mbalimbali ili waendelee kupata uzoefu hiyo itasaidia kuipunguzia serikali gharama ambazo imekuwa ikitumia kutoa tenda kwa kampuni za nje ya nchi.
"Ni vyema wakandarasi wazawa wakawa wanahusika moja kwa moja katika kutekeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchi hiyo itasaidia serikali kutumia fedha kidogo na kupata uzoefu kutoka kwa wakandarasi wa kigeni,"amesema.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa ACCT Profesa Mhandisi John Bula alisema wamendaa kongamano kubwa litakalofanyika katika ukumbi wa Jakaya kikwete Dodoma lengo ni kutoa pongezi kwa Rais Samia kwa kutwaa tuzo ya heshima.
Amesema Mgeni rasmi katika kongamano hilo ni Waziri wa ujenzi na uchukuzi Makame Mbarawa.
Kesho ni pongezi kubwa kwa Rais wetu kwa kupata tuzo kubwa ambayo inatupa nguvu kwasababu hata sisi wakandarasi wazawa ameendelea kutujali kwa kutupatia kazi mbimbali za ujenzi tunachoomba tupewe fursa zaidi ili tuonyeshe uwezo zaidi kwasababu utaalamu unaweza ukanunuliwa kutoka nje kwa pale tutakapokwama,"alisema
Naye Mwanachama wa ACCT Maida Waziri amesema tuzo aliyoipata Rais Samia ni tuzo kubwa watanzania hawanq budi kuendelea kutambua na kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katika sekta ya miundombinu.
Amesema kupitia tuzo hiyo Dunia imeweza kumtambua hivyo kama watanzania lazima kutambua umuhimu wa kile alichopewa Rais Samia na kutembe kifua mbele kwasababu haikuwa kazi rahisi kuchukua tuzo hiyo.
Tuzo hiyo ameipata kutokana na ujenzi wa miundombinu kwa kweli tuna haki ya kujivunia sana kwa sababu kama watanzania Rais Samia ameleta tuzo hiyo kubwa napenda kusema kuwa watanzania tunaona dira na muelekeo wa serikali ya awamu ya sita tunaona njia kubwa huko tunakoenda
Maida amesema kigezo cha nchi kuonekana ni tajili mara nyingi hupimwa kwenye ujenzi wa miundombinu na kwa tuzo hiyo ambayo Rais Samia ameipata ameonyesha watanzania kuwa Tanzania ni nchi tajiri.
"Rais Samia amepewa tuzo na Benki ya Afrika imetambua jitihada anazozifanya katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo miradi aliyoikuta iliyoanzishwa na hayati Dk.John Magufuli na kuanzisha miradi mipya,"ameeleza
0 Comments