📌MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Francis Michael,amepokelewa na watumishi wa Wizara hiyo huku akiwaahidi ushirikiano na kusimamia masuala yote yanayohusu elimu nchini.
Akiwasili leo Juni 20,2022 katika Ofisi yake Mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma mara baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu hivi karibuni.
Dk.Michael ambaye alishatumikia taasisi mbalimbali za elimu ikiwemo chou kikuu cha Dar es Salaam kama Mkufunzi,ameomba ushirikiano kwa watumishi wa Wizara hiyo katika kusimamia wizara hiyo huku akiahidi kutoa haki sawa kwa wote.
Katibu Mkuu huyo amesema katika muda wa utumishi wake katika Wizara hiyo atahakikisha kuendeleza yote mazuri ya watangulizi wake huku wakiwaomba watumishi aliojitokeza kumpokea kuchapa kazi.
Masuala ya watumishi hamtapata shida lakini kila mtu lazima atekeleze wajibu wake, sitakuwa na mzaha kwa wale wanaokwamisha mambo ndani ya Wizara, tufanye kazi kama timu ili tutimize malengo
Dk.Michael
Pia amesema kuwa atawasiliana na wizara ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kupata maeneo ambayo yanahitajika kuweka mkazo mkubwa katika kuhakikisha wanafunzi wanasoma kada hiyo ili kupunguza uhitaji uliopo .
“ Nitapita kwenye mipango na malengo ya wizara ili kuhakikisha sitoki nje ya malengo yaliyopo na mnaona hivi karibuni tu Rais wetu Samia amepitisha Elimu bure kwa kidato cha tano na sita kikubwa ni kulinda maono na ile ndoto njema ili kuifikisha Elimu ya Tanzania katika eneo salama “Amesema Dkt.Michael
Hata hivyo amesema kuwa moja ya mikakati yake ni kuendeleza mchakato wa kuboresha mitaala ya elimu sambamba na kuimarisha vyuo vya kati ili kuziba pengo la mahitaji ya taaluma na ujuzi yaliyopo.
Najua Wizara ya Utumishi imefanya
uchambuzi kujua mapengo gani ya taaluma ambayo yanatakiwa ili kuziba na mitaala
inatakiwa kulenga huko
Dk.Michael
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amemhakikishia ushirikiano mkubwa katibu huyo Mpya huku akisema kuwa watendaji wa wizara hiyo ni wachapa kazi hivyo atafurahia uwepo wake ndani ya timu hiyo mpya.
Kipanga amesema kuwa kuna haja ya kufanya kazi kama timu Iii kufikia malengo ya wizara na kuwatumika wananchi katika sekta ya elimu.
Nakuhakikishia kuwa hapa ulipokuja ni kama nyumbani kwako na hawa unaowaona mbele yako ni majembe kweli kweli naongea hivyo nikiwa na uhakika mkubwa kuwa utafurahia uwepo wako hapa Kipanga
0 Comments