📌RHODA SIMBA
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi amewataka wafanyakazi wa sekta ya Mawasiliano nchini kukuza maarifa na kuwa na uchumi shindani wa kidijitali ili kuwa kitovu cha watu kujifunza namna ya kutafuta fursa katika taasisi za kimataifa.
Akizungumzia leo June 21 jijini Dodoma katika kikao kazi cha uchambuzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya Mawasiliano kitaifa na kimataifa Jimmy Yonazi amesema kuwa Wizara ya Mawasiliano imekusudia kufungua ajira kwa watanzania kitaifa na kimataifa ili kuwa nchi yenye fursa nyingi lengo likiwa nchi zingine nazo zije kujifunza hapa nchini.
Lengo letu ni kufungua ajira kwa watanzania kitaifa na kimataifa Ili kuwa na nchi yenye fursa nyingi Ili nao watu wa mataifa wengine waje wajifunze kutoka hapa mchini kwetuDkt.Yonazi
Aidha Yonazi amesema kila mmoja atambue jukumu lake siyo kuja ofisini na kurudi nyumbani tu ambapo amewasisitiza kufanya kazi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kimataifa.
"Kila mmoja akitambua jukumu lake amekuja hapa kufanya nini tutapiga hatua hata kwa mataifa mengine"amesema Yonazi
Kwa upande wake mkurugenzi wa TEHAMA Kutoka Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku amesema kuwa watatekeleza maagizo ya Serikali ili kuongeza ajira pamoja na pato la Taifa.
"Tutaenda kutekeleza yale tuliyoelekezwa na Serikali na niseme tu tutafanya kwa weledi ili kuhakikisha ajira na Pato la Taifa linaongezeka" amesema Munaku.
0 Comments