📌RHODA SIMBA
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kutoka orodha ya majina ya makarani na wasimamizi wa sensa ya watu na makazi ikisema orodha hiyo siyo ya kweli na bado mchakato wa kupitia maombi bado unaendelea. .
Taarifa hiyo imetolewa Leo Mei 27 jijini hapa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema taarifa hizo siyo rasmi kwa watanzania waliyo omba nafasi za ukarani na usimamizi wa Sensa katika maeneo wanayoishi.
Dkt.Chuwa amesema muda wa maombi kwa nafasi hizo za kazi ulifika tamati tarehe 19 Mei ambapo idadi ya waombaji ilifikia 689,935 kati ya 205,000 wanaohitajika kwenye zoezi la sensa kwa mwaka 2022.
Watu hawa ambao hawana nia nzuri kwa Serikali na watanzania kwa ujumla wamekwenda mbali na kutamka tarehe ya usahili kuwa ni 29 Mei 2022, napenda ifahamike kwamba mchakato wa ajira za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa bado unaendelea katika ngazi ya kata, shehia na Halmshauri zoteDkt Chuwa.
Amesema zoezi la uchambuzi wa maombi kwa waombaji wote linatarajiwa kuanza tarehe 02 Juni 2022 kwenye Kila kata au shehia husika baada ya kukamilika kwa mafunzo ya maafisa watakaohusika kufanya usahili.
Mchakato wa ajira za makarani na wasimamizi wa sensa linakwenda vizuri kulingana na ratiba ya sensaDkt Chuwa
Hata hivyoo Dk Chuwa amewataka wananchi kwamba taarifa yoyote kuhusu mwenendo wa maandalizi ya sensa ya watu na makazi sensa ya majengo na sensa ya anwani za makazi ikiwemo ajira za muda zitatolewa na Serikali kupitia vyombo vya habari.
0 Comments