📌RHODA SIMBA
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Watoto(UNICEF) limetoa Vishikwambi 830 kwa Serikali kwajili ya kutekeleza zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu.
Akizungumza Leo April 25 jijini hapa Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka huu na Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda amesema kwa mara ya kwanza Tanzania inaendesha zoezi hilo kwa njia ya kidigitali ikiwemo matumizi ya kutumia vifaa vya kisasa kama Vishikwambi.
"UNICEF wametuokoa unaweza usione umuhimu wa vishikwambi hivi lakini tunashukuru sana kwasababu temepanga kufanya Sensa ya kidigitali ambayo haitatumia makaratasi kwa muktadha huo vishikwambi hivi vilikuwa vinahitajika,"amesema.
Awali akitoa salamu Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa amesema Sensa ya mwaka huu itafanyika kidigitali kwa mara ya kwanza haitotumia makaratasi hivyo itatumia vishikwambi katika kukusanya na kutunza taarifa.
Amewapongeza wadau hao ambao wameunga mkona serikali na kuwahamasisha wadau wengine kujitokeza Kwa wingi kuungana na serikali ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika Kwa kisasa na kirahisi zaidi.
Sensa inaenda kufanyika kidigitali ambayo haitatumia makaratasi matumizi ya vishikwambi ni muhimu kwasababu vitarahisisha kazi ya ukusanyaji taarifa na kufanya Tanzania kuingia katika orodha ya nchi chache ambazo zinatumia teknolojia hiyo
Naye Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar Abdulmajid Jecha amesema Dunia sasa imebadilika imeanza kufanya mambo yake kidigitali na Tanzania haina budi kubadilka na kuelekea huko
Amesema Duniani kote ukusanyaji wa taarifa na takwimu za vitu mbalimbali zimeanza kufanyika kwa kutumia njia za kidigitali ikiwemo matumizi ya vishikwambi na wamefanikiwa
"Vishikwambi hivi vitasaidia kukusanya taarifa Kwa urahisi zaidi tutaona kama ni vidogo lakini ni vya maana sana na tunaomba na wadau wengine wajitokeze kutoa vifaa kama hivi au vingine ili kurahisisha kazi,"amesema.
Naye Mwakilishi wa (UNFPA) Tanzania Dk. Majaliwa Marwa alisema wamekuwa wakishirikiana na Tanzania katika shughuli za sensa ya watu na makazi tangu ilipotangazwa kuwa itafanyika kidigitali ambapo hadi sasa maandalizi yamefikia asilimia 80.
Nawapongeza wenzetu wa UNICEF ambao leo wanatoa vifaaa na natoa wito kwa wadau wengine kutoa mchango wa jali na mali Kwa serikali ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa huku wananchi wakiendelea kuhamasishwa na kupewa elimu juu ya ujio wa sensa ya watu na makazi
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Dk. Shalini Bahunguna, UNICEF aliipongeza serikali Kwa dhamira yake ya kutekeleza sensa ya watu na makazi Kwa kidigitali zaidi na kuwataka watanzania kuwa tayari kushiriki zoezi hilo
Amesema Sensa ni muhimu kwa Taifa katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
0 Comments