TANGA NA DAR ES SALAAM YATAJWA KUTOFANYA VIZURI UWEKAJI ANUANI ZA MAKAZI

 

📌RHODA SIMBA

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameitaja mikoa ya Tanga na Dar es Salaam kuwa bado haijafanya vizuri kwenye uwekaji wa anuani za makazi.

Nape ametoa kauli hiyo leo April 11 akiwa katika uwanja wa ndege jijini Dodoma wakati anaanza safari ya kuzunguka nchi nzima kufanya uhamasishaji wa uwekaji anuani za makazi.

Tathmini yetu inaonesha tumefikia asilimia 68 na 69 lakini bado kuna maeneo yana changamoto ikiwemo mikoa ya Dar es salaam na Tanga lakini kuna mikoa inayofanya vizuri ikiwemo mkoa wa Lindi na mikoa mingine sasa kwa kuwa muda umeisha inabidi tuongeze nguvu 

Nnauye

Amesema shughuli hiyo ya uwekaji wa anuani za makazi nchini inatakiwa kuhitimishwa Mei 22, 2022 ingawa kwa sasa imefikia wastani wa asilimia 68 kwa nchi nzima.

Nguvu ya kuongeza hamasa na ukaguzi kwenda kuona katika maeneo unaahitajika mfumo unaonesha ukusanyaji wa taarifa na upamdishaji na uwekaji wa alama na namba ambayo ndio kazi yenyewe leo tunaanzia Tanga asubuhi Kilimanjaro mchana na Arusha jioni na zoezi hili litakuwa la nchi nzima

Nnauye

Waziri akiwa na timu yake wameanza ziara hiyo mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha huku akisema kwamba katika baadhi ya maeneo wanalazimika kuongeza nguvu katika  kupeleka wataalamu zaidi.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments