📌RHODA SIMBA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta huku bei za jumla na rejareja za petrol, dizeli na mafuta ikionekana kupanda .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Petrol Gerald Maganga amesema bei za jumla za petroli zimeongezeka kwa shilingi 320 kwa lita sawa na asilimia 13.3, dizeli umeongezeka kwa shilingi 288.50 kwa lita sawa na ongezeko la asilimia 12.6 huku mafuta ya taa yakiongezeka kwa shilingi 472 kwa lita.
“Bei za jumla na rejareja za mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia bandari ya dar es salam zimeongezeka ikilinganishwa na mwezi ulioisha kwa upande wa petroli imeongezeka kwa shilingi 321 ambayo ni asilimia 12.6, dizeli shilingi 289 huku mafuta ya taa yakiongezeka kwa shilingi 474 kwa lita ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 21.4,”amesema Maganga
Maganga amesema bei za jumla na rejareja za mafuta kwa mikoa ya kaskazini Tanga,Kilimanjaro, Arusha na Manyara zimeongezeka ikilinganishwa na mwezi uliopita.
Amesema kwa mwezi huu bei za rejareja za petroli,dizeli na mafuta ya taa katika mikoa hiyo ya kaskazini zimeongezeka kwa shilingi 285 kwa lita (Petroli), sawa na asilimia 11.1, shilingi 295 kwa lita (Dizeli) sawa na asilimia 11.9 mfulululizo.
“Vile vile ikilinganishwa na toleo la mwezii la mwezi uliopita bei za jumla za petroli na dizeli zimeongezeka kwa shilingi 284.22 sawa na asilimia 11.68 na shilingi 294.66 lita sawa na asilimia 12.52.”amesema Maganga
Amesema waendeshaji wa vituo vya mafuta vilivyopo kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es salaam na hivyo bei za reja reja za mafuta ya taa kupitia bandari ya Dar es salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.
Hata hivyo amesema kwa mwezi machi bandari ya Mtwara imepokea mafuta ya dizeli pekee na kwa mwezi april 2022 bei za reja reja na jumla za mafuta ya petroli kwa mikoa ya kusini mtwara na lindi zimekuwa sawa kama zilivyotangazwa mwezi Machi.
0 Comments