📌RHODA SIMBA
WAKATI zoezi la utambuzi wa maeneo katika Jiji la Dodoma likitarajia kuanza kesho tarehe 23 Machi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imewataka watendaji wa Kata na Mitaa kuwasaidia waweze kuweka alama za mipaka ya mitaa ili zoezi hilo liweze kufanyika kwa ufanisi mkubwa.
Hayo yameelezwa leo Jijini hapa na Mratibu wa Sensa Taifa,Seif Kuchengo wakati akiwasilisha mada kwa watendaji wa mitaa,watendaji wa Kata Maafisa tarafa,pamoja na madiwani,kwenye mkutano wa maandalizi ya utengaji wa maeneo ya kuhesabia watu.
“tupate idadi ya kaya katika mtaa ,tupate makadirio au makisio ya idadi ya watu waliopo katika mtaa, na jukumu lingine ni kuwapitisha wataalam katika mipaka sahihi bila kuachaa eneo la mitaa kwasababu kumekua na changamoto kaya zingine zinakuwa hazipo kwenye mipaka ila zinapata huduma” amesema Kuchengo
Kwa upande wake,Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Tanzania Bara,Anne Makinda amesema katika zoezi la utambuzi wa mitaa Mkoa wa Tanga umekuwa kinara kwa kupangwa vizuri hivyo amewaomba watendaji hao kuisaidia timu ya wataalamu ambayo itapita kesho katika maeneo yao ili waweze kupata mipaka sahihi kwani sensa hiyo italeta maendeleo kwa Nchi .
Sensa ni kwaaajili ya maendeleo yetu na hata mahangaiko ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan hapa yatajibiwa kwa sensa hii kwahiyo kila mtu ahakikishe anatoa kampeni ya sensa lakini pia yeye na familia yake ahakikishe wanahesabiwa
Makinda
Naye Kamisaa wa Sensa Tanzania Visiwani,Balozi Mohammed Haji Hamza ameomba ushirikiano kwa watendaji hao ili kufanikisha zoezi la sensa kwani zoezi la utambuzi likikamilika litafuatia zoezi la mafunzo, kuaandaa vifaa na kuajiri watu.
Naye Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali,Ruth Minja amesema kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika kwa asilimia70 yakiwemo madodoso miongozo na sensa hiyo itatarajia kufanywa kwa njia ya kidigitali tofauti na kipindi cha nyuma.
0 Comments