NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA ARIDHISHWA NA UENDESHWAJI WA CHUO CHA MIPANGO



📌RHODA SIMBA

NAIBU kaibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Jenifa Omolo ameridhishwa na utendaji kazi wa uongozi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP)  ikiwemo kuhakikisha wanalipa madeni ya watumishi na matumizi bora ya fedha

Ameyasema hayo leo ijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Kamati ya uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) sambamba na kukagua miradi ya ujenzi wa kampasi kuu ya Dodoma.

Akizungumza na kamati ya uongozi amesema wataalamu wa chuo hicho wanatakiwa kuwa chachu ya mipango ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi katika mipango wanayohihitaji.

Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ni kati ya vyuo ambavyo vinatazamiwa kwa kufanya mipango mizuri ya maendeleo kwa kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa sambamba na kuwashirikisha wananchi mipango ambayo wataifanya 

Jenifa.

Wataalamu lazima wajiulize kuwa wanaenda kubadiisha nini katika jamii,kila tunachokipanga kiwe na manufaa kwa wananchi na kuwashirikisha pamoja na vipaumbele vyake

 Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Mipango Profesa Hozen Mayaya amesema chuo hicho kimefanikiwa kukusanya sh.bilion 18.9 ikiwa ni asilimia 84 ya lengo la kukusanya sh.bilion 22.5 Kwa kipindi cha Julai hadi Februari 2022.

Katika hatua nyingine Profesa Mayaya alisema chuo hicho kimefanikiwa kulipa madeni ambapo hadi kufikia Februari 28 mwaka huu sh.bilion 2.6 zimelipwa kati ya deni la sh. bilion 3.1.

Amesema kati ya madeni yaliyolipwa madeni ya wafanyakazi ni sh.bilion 1.6 na madeni ya watoa huduma ni sh. Milion 995.3 ambapo hadi kufikia Machi mwaka huu chuo kinadaiwa sh. milion 426.9 ambapo kati yake sh.milion 330.2 ni ya wafanyakazi na sh.milion 96.8 ni kwàajili ya watoa huduma.

Chuo kimeweka mikakati wa kuhakikisha kila mwezi kulipa deni hili kwa sh.milion 106.8 ili kuhakikisha deni hili linamalizika ifikapo Juni 30 mwaka huu

Profesa Mayaya aliongeza kuwa kwa sasa chuo kinatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kumbi tatu za mihadhara, ujenzi wa mabweni mawili, ujenzi wa mgahawa Kitumba Magu, ujenzi wa jengo la utawala Kitumba Magu na kununua ardhi kwàajili ya upanuzi wa chuo  ambapo sh.bilion 10.9 zimetumika kugharamia miradi hiyo.

Amesema kati ya fedha hizo zilizotumika sh. bilion 7.7 ni ruzuku kutoka serikali kuu na sh. bilion 3.2 ni mapato ya ndani ya chuo.

Miundombinu ya kufundishia na ofisi zilizojengwa zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 2400 na wafanyakazi 102 kwa wakati mmoja na miundombinu ya malazi itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 408 Kwa wakati mmoja

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo Cha Mipango Martha Qorro alisema ziara ya Naibu katibu Mkuu imekuja wakati muafaka wakiwa katika mafanikio ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.




Alisema wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kusimamia chuo ili kuboresha mazingira kuwa rafiki kwàajili ya kujifunzia na kufundishia kwa kuwa na miundombinu bora na ya kisasa zaidi.

Kama alivyotangulia kusema mkuu wa chuo kuwa tunaendelea na ujenzi katika kampasi zote mbili ya Mwanza na Dodoma na tunatoa shukrani kwa serikali kwa kutuwezesha fedha kwàajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi yetu ambayo itakuwa na manufaa kwa wanafunzi na Taifa kwa ujumla

 MWISHO..


Post a Comment

0 Comments