DKT. CHAULA AIOMBA TBA KUHARAKISHA MCHORO WA JENGO LA WIZARA
March 10, 2022
📌WMJJWM
KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewaomba Wakala wa
Majengo ya Serikali (TBA) kuharakisha taratibu za kupata mchoro wa jengo la
Ofisi za Wizara hiyo ili ujenzi uanze mapema.
Dkt. Chaula ametoa kauli hiyo wakati akipokea
kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Wizara, katika Mji wa Serikali Mtumba,
Jijini Dodoma tangu kuundwa kwa Wizara hiyo mpya ambapo kabla ilikuwa ni sehemu
ya Wizara ya Afya.
Amesema TBA ifanye jukumu lake la kuhakikisha
mchakato wa ujenzi unakamilika kwa wakati hivyo kuwezesha Wizara kuendelea
kuhudumia wananchi kwa sababu inagusa makundi yote katika jamii ikiwemo makundi
maalum.
Kikubwa tunakimbizana na muda, kwa hiyo
tumeshakabidhiwa eneo hili, hivyo wenzetu wa TBA watoe michoro ili ujenzi uanze
kwani Wizara hii ni mtambuka
Dkt. Chaula
Kwa upande wake, Mratibu wa ujenzi wa Mji wa
Serikali Meshack Bandawe amesema kutokana na mahitaji ya Wizara hiyo kwa ukubwa
wake kulikuwa na umuhimu wa kuwa na eneo lake na jengo kamili ili kurahisisha
shughuli zake na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ili kukidhi mahitaji ya
Serikali kwa miaka ijayo.
Kwa hatua hii tunatarajia jengo la
Wizara hii litakuwa miongoni mwa majengo 25 yatakayojengwa hapa Mtumba, mara
baada ya taratibu za kimamlaka kukamilika
Bandawe.
Naye Msanifu majengo kutoka TBA Ngh'olo Weja
amesema TBA itatahakikisha mchoro wa majengo hayo, unakamilika mapema kwa
kufuata sheria pamoja na taratibu zote za kumpata mkandarasi.
MWISHO
Post a Comment
0
Comments
Hey there, We are Blossom Themes! We are trying to provide you the new way to look and use the blogger templates. Our designers are working hard and pushing the boundaries of possibilities to widen the horizon of the regular templates and provide high quality blogger templates to all hardworking bloggers!
0 Comments