BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WATANGAZA MATOKEO YA MITIHANI

 

📌RHODA SIMBA

MKURUGEZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfrey Mbanyi ametangaza matokeo  ya mitihani ya 23  huku akisema ufaulu  ni asilimia 34.6 huku wastani wa ufaulu kuonekana siyo mzuri .

Akiongea leo jijini Dodoma na waandishi wa habari Mkurugenzi mtendaji huyo amesema katika mtihani huo wa 23 walidahili watahiniwa 479 na walioweza kufanya mitihani 427 na watahiniwa 28 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

Amesema mitihani hiyo ilifanyika Januari mwaka huu ambapo baada ya kusahishwa na kuchakatwa kwa mitihani hiyo matokeo yalionesha watahiniwa 156 kati ya watahiniwa 451 waliofanya mitihani wamefaulu hiyo ni sawa na asilimia 34.6 ya watahiniwa wote waliofanya mitihani.

Katika Mitihani hiyo watahiniwa 230 watakuwa na mitihani ya marudio baada ya kufaulu somo moja au mawili kwenye masomo yao kwahiyo watapewa nafasi ya kurudia tena masomo yao

Mkurugenzi 

Amesema Watahiniwa 65 sawa na asilimia 14.4 hao wamefeli na wanatakiwa kurudia masomo yote na watatangaziwa muda wa kurudia masomo hayo.

Hata hivyo amesema kwenye mitihani hiyo kuna mambo yalijitokeza wamekuwa wakiona mitihani yanayojumuisha mahesabu mambo ya takwimu na uchumi kumekuwa na tabia ya watahiniwa kufeli lakini katika mitihani hiyo ya 23 masomo ya taaluma yanayohusu Ununuzi na Ugavi  watahiniwa wamefeli sasa hiyo ni changamoto kwani hayo ndio maeneo yao watakayoenda kufanyia kazi.

Kitendo cha kufeli kiasi hicho kinaipa bodi jukumu la kuweka mikakati ya kuhakikisha watahiniwa wanaelewa wanacho fundishwa na kuweza kufauli vizuri mitihani yao  

Pia amesema wamaejaribu kuangalia katika masomo yote watahiniwa walifanya masomo 32 masomo 6 waatahiniwa walifanya vibaya na masomo 17 walifaulu wastani na masomo yalibaki walifanya vizuri kiasi chake kwahiyo ufaulu wa asilimia 34.6 kwa ujumla matokeo si mazuri .

Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi imeweka mikakati ya kuwasaidia watahiniwa wao kwa kuhakikisha vituo vyao vya kujiandaa na mitihani vinasimamiwa vizuri vikiwa na walimu wanao fundisha na wenye uwezo pamoja sifa stahiki ili kuboresha uelewa wa wanafunzi wanapokuwa vyuoni na hatimaye uelewa huo uweze kuwasaidia wanapokuja kufanya mitihani ya kitaaluma.

 Kitendo cha kutangazwa kwa matokeo hayo   sasa wanatangaza mitihani ya 24 waanze kujisajili na usajili unafanyika kwa njia ya mtandao hivyo waje kujisajili na wale wanaotakiwa kurudia mitihani wajiandae kwa mitihani hiyo


Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ni taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 23 mwaka 2007 kwaajili ya kusimamia  tasnia nzima ya Ununuzi na Ugavi hapa nchini. 

 MWISHO

Post a Comment

0 Comments