BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI YATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI

 

📌RHODA SIMBA

SERIKALI imetoa wito kwa bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi PSPTB kusimamia sheria iliyoianzisha bodi hiyo kwa kujumuisha usimamizi wa maadili,mienendo ya wataalamu na utengenezaji wa mitaala inayozingatia umahiri wa kitaalamu na mahitaji ya soko.

 Akizungumza Leo Machi 9 Jijini hapa kwenye uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Lawrance Mafuru amesema kuwa uandaaji na usimamizi wa miongozo mbalimbali inayohusu taaluma na kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu taaluma zitatoa majibu kwa changamoto zinazojitokeza kwenye taaluma hiyo.

 Kadhalika amewaasa waajiri kutoa taarifa kwenye bodi zinazohusiana na ukiukaji wa maadili kwa wataalamu ili hatua sitahiki ziweze kuchukuliwa kwani hakuna ufanisi bila maadili na weledi.

Hakikisheni waajiri wote wanaajiri watumishi wenye Sifa sitahiki zinazotambuliwa na Sheria ya PSPTB na kuzingatia mahitaji yaliyopo kwenye waraka wa Maendeleo ya utumishi namba 3 wa mwaka 2015 wa kada zilizopo chini ya Fedha na Mipango,

 Katibu.

 

Pia amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kusaidia bodi hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na usimamizi mzuri wa Rasilimali watu pamoja na matumizi sahihi ya rasilimali fedha ili malengo yaliyopangwa yaweze kutekelezwa kwa ufanisi

Nawasisitiza kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira ya utulivu wa kutosha ili waweze kutoa tija kwenye utendaji wao Mimi pamoja na viongozi wangu wa Wizara tuna imani kubwa kwenu katika kutekeleza haya.

Katibu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi PSPTB Jacob Jail Kibona amesema kuwa bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi,imepewa jukumu la kusimamia misingi ya taaluma ya Ununuzi na Ugavi na mienendo ya wataalamu wake.

Aidha amesema kuwa bodi inawajibu wa kuzalisha wataalamu wenye weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma yao.

Bodi hii pia inajukumu la kuishauri Serikali kuhusu taaluma ya Ununuzi na Ugavi ili kuleta tija katika kutumia rasilimali za Serikali, 
Naahidi kuwa bodi yangu itasimamia na kuimarisha taaluma ya Ununuzi na Ugavi sambamba na kuongeza nguvu ya kupambana na vitendo vyote vinavyokinzana na maadili ya kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi kama ubadhirifu wa Mali, Rushwa na ukiukaji wa taratibu za Ununuzi na Ugavi

Mwenyekiti.


Hata hivyo bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi imepewa jukumu la kusimamia misingi ya taaluma ya ununuzi na Ugavi na mienendo ya wataalamu wake,pamoja na kuzalisha wataalamu wenye weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma yao.

 Mwisho.

Post a Comment

0 Comments