📌HAMIDA RAMADHAN
WAZIRI wa Afya Ummy mwalimu amewataka wanaume kuacha kuogopa kupima Saratani ya Tezi Dume kwani kuna vipimo vipya na vya kisasa tofauti na ile njia ya upimaji wa zamani .
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akitoa tamko katika maadhimisho ya siku ya saratani Duniani kwa mwaka 2022 yenye kauli mbiu isemayo 'huduma za saratani sawa kwa wote'
Waziri Ummy amesema maendeleo ya teknolojia yanaruhusu ubunifu wa njia mpya za upimaji hivyo amewataka wanaume wenye umri kuanzia miaka 40 kwenda kwenye vituo vya afya kutafuta huduma hizo ili kujiweka salama na kansa ya tezi dume.
Katika kansa ambazo zinawaathiri sana wanaume ni tezi dume,lakini cha ajabu wamekuwa waoga kwenda kupima.Rai yangu kwao wajitokeze kupima ili kama wakigundulika mapema wapatiwe matibabu kwa haraka ili kuokoa maisha.
Vipimo vitakuwepo katika vituo vyote kuanzia ngazi za kutolea huduma za afya ambapo amesema pia wanaume wamekuwa wakikabiliwa na saratani ya Tezi dume asimilia 21 saratani ya Koo kwa asilimia 11.8 Kinywa na mdomo kwa asimia 7.3 Utumbo mdogo asilimia kwa asilimia 9 na mkubwa.
Amesema kwa upande wa wanawake saratani inayowaathili zaidi ni saratani ya kizazi kwa asilimia 43 saratani ya matiti 14.2 na Saratani ya koo kwa asilimia 3 .8
"Na ndio maana nasema kama tukifanikiwa kupunguza saratani ya Mlango ya kizazi maana yake tutapunguza wagonjwa wa saratani kwa asilimia 40," Amesema
Na kuongeza kuwa "Ugonjwa wa saratani na
magonjwa mengine yasio ambukiza yanachangiwa na mtindo wa maisha kama vile
ulaji mbaya, kutokufanya mazoezi.
0 Comments