📌JASMINE SHAMWEPU
SERIKALI ina Mpango wa
kuanzisha masjala ya hewa ya ukaa itokanayo na misitu ili kuchangia
uchumi wa nchi.
Hayo yamebainishwa
jijini Hapa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro wakati
akishiriki zoezi la Upandaji wa miti katika eneo la Iyumbu ikiwa ni mwendelezo wa
maadhimisho ya wiki ya Sera mpya ya Mazingira ya mwaka 2021 inayotarajiwa
kuzinduliwa Februari 12,2022 na Makamu wa Rais Dkt.Philiph Mpango.
Dkt.Ndumbaro amesema kuna faida kubwa itokanayo na misitu
hivyo mkakati wa serikali ni kuhakikisha misitu inalindwa na kuhamasisha
upandaji wa miti zaidi.
Amesema Misitu inachangia pato la taifa asilimia 3.5 inazidi
sekta nyingine ambazo watu hawajui ndio maana tunasema Misitu ni Mali watu
wanafanya Biashara ya mbao, Biashara ya thamani bila kusahau Misitu ndio chanzo
cha Mazingira mazuri tuliokuwa nayo.
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Andrew Komba
amesema zoezi la kujanikisha Dodoma kwa upandaji miti linaratibiwa na
Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Pia amesema Februari 10,2022 Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira itatoa elimu kwa jamii katika soko la Chang’ombe namna
nzuri ya urejeshaji wa taka ngumu kwa ajili ya matumizi mengine.
Meneja wakala wa misitu Tanzania [TFS] Prof.Santos Silayo
amesema amezungumzia faida ya misitu ni pamoja na kuleta mapinduzi makubwa ya
viwanda ambapo zaidi ya viwanda 800 vimeanzishwa.
Ikumbukwe kuwa kabla ya kupitishwa sera mpya ya Mazingira ya
Mwaka 2021, sera ya Mazingira iliyokuwa ikitumika ni ya mwaka 1997 ambayo
imedumu takribani miaka 25 kabla ya kuhuishwa tangu kuanzishwa kwake.
MWISHO.
0 Comments