SERIKALI KUBORESHA UTENDAJI KAZI SUALA LA ULINZI NA USALAMA WA MITANDAO




 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

KATIBU Mkuu Wizara ya habari,Mawasiliano  na teknolojia ya Habari Dk Jimmy Yonazi amesema, Serikali  itahakikisha  inaboresha ushirikiano na mataifa ya nje katika utendaji kazi kuhusu suala zima la ulinzi na usalama ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kimtandao.

Ameyasema hayo leo  Februari 24 Jijini hapa wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wapelelezi pamoja na maaskari wa chumba cha mashtaka wa Tanzania na Zanzibar lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya uhalifu wa Mtandao.

Aidha Dk.Yonazi amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu  kwaajili yakujenga uwezo wa nchi hivyo jukumu lao ni   kuhakikisha wanalinda usalama wa nchi.

Kama Serikali tutaendelea kufanyia kazi ya mashirikiano baina ya nchi yetu na nchi nyingine katika kuhakikisha tunaimarisha masuala ya mawasiliano ya TEAHAMA ili kukabiliana na uhalifu wa kimtandao

Pamoja na mambo mengine amesema uhalifu wa kimtandao ni mpana na kila siku teknolojia inakuwa hivyo ni muhimu kuhakikisha kila mara wanajengeana uwezo ili kwenda na ulimwengu wa kidijitali.

Amesema Serikali imechukua hatua kwa kutunga Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka  2015 ili kuweza  kukabiliana na masuala ya uhalifu wa kimtandao ambao umekuwa ukishika kasi.

 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini,DCI Camilius Wambura amesema Mafunzo hayo yataleta matokeo chanya kutokana na mbinu walizopata ili kukabiliana na uhalifu wa kimtandao kwani maarifa yatawasaidia katika kubadilishana taarifa.

Wambura amewataka wapelelezi hao pamoja na askari kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na nidhamu katika utendaji kazi wao  kwani tabia za wachache zimekuwa zikiharibu taswira ya Jeshi jambo ambalo si jema.

 

Post a Comment

0 Comments